Wabaptist: Utengano wa Kanisa na Utawala wa Nchi

“…Mlipeni kaisari yaliyo ya kaisari;
na Mungu yaliyo ya Mungu.”
Mathayo 22:21

Akizungumza kutoka kwenye Mji Mkuu wa Marekani mwaka 1920 mbele ya watu 15,000 kwenye eneo la wazi, Mchungaji wa Texas Baptist  George W. Truett alisema: “‘Mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari na Mungu yaliyo ya Mungu,’ ni moja ya mapinduzi na matamshi ya kihistoria yaliyowahi kutoka kwenye kinywa cha mcha Mungu. Hilo tamko, moja na la mwisho, kulifanya utengano baina ya Kanisa na Serikali… ilikuwa silaha ya machweo ya hiyo siku, muango ambao unapaswa kuendelea zaidi na zaidi kwenye kila ardhi, iwe kubwa au ndogo, fundisho hili litakuwa na heshima ya hali ya juu mahali lilipo Kanisa huru kwenye nchi huru..”

Misngi wa Kanisa huru kwenye Nchi  huru

Kwa Wabaptist, dhana ya Kanisa huru na nchi huru sio tu kwa ajili ya suala la kisiasa au kwa yale yaliyoandikwa na mwanadamu lakini kwenye Neno la Mungu. Imani ya Baptist juu ya uhuru wa dini na masuala yake, utengano wa taasis za Kanisa na nchi, kulitokana na msimamo wa Baptist juu ya mamlaka ya Biblia.

Ni nini maana ya ‘Kanisa” na “nchi”? Neno “nchi” lina maana ya serikali. Biblia inasema serikali zimewekwa na Mungu ili kuitisha nchi kwa sheria na taratibu (Warumi 13:1-5). Viongozi wa serikali hupaswa kutenda kwa faida ya wananchi (1 Petro 2:13-14). Wabaptist na Wakristo wengine hupaswa kuheshimu na kuwaombea viongozi wa serikali (1 Timotheo 2:1-3; 1 Petro 2:17), kulipa kodi (Mathayo 22:17-22; Warumi 13:6-7) na kuitii serikali isipokuwa huo utii utakuwa ni kinyume na kusudi la Mungu (Matendo 4:19-20; 5:29). Kihistoria, Wabaptist wamekuwa wanyenyekevu kwa mamlaka ya nchia.

Neno  “Kanisa” maana yake ni taasis ya kidini. Kwa Wabaptist, ni pamoja na Kanisa la mahali na ngazi mbalimbali zilizopo kwa nia ya kukamilisha shughuli za kidini, mfano majimbo, kanda, mashule na taasis mbalimbali zenye huduma. Wabaptist hufundisha kusudi la “Kanisa” ni kueneza injili ya Yesu Kristo (Matendo 1:8), kufundisha imani na kutengeneza waumini wapya (Mathayo 28:19-20; Waefeso 4:11-13) na kuhudumu kupitia jina la Kristo (Mathayo 25:31-46).  Kanisa linapaswa kutegemea msaada wa Kiroho na sio msaada kutoka serikalini ili kuendesha huduma zake.

Ni sawa, uhusiano katika ya Kanisa na serikali ni wenye faida. Kwa mfano, nchi inapaswa kutoa sheria na usalama, haya ni muhimu sana kwa Kanisa ili kufanya huduma zake vizuri (Matendo 13-16). Na Kanisa huchangia kwa kuwa na jamii bora kwa kusaidia kutii sheria, kufanya kazi kwa bidii, na kuwa raia waaminifu (Waefeso 4:24-32; 1 Petro 2:11-17).

Wabaptist huamini hizi faida kwa pande zote hufanya vema kama taasis za Kanisa na nchi vimetengana bila kwa kila upande kuingilia upande mwingine. Nchi haina mamlaka ya kuingilia masuala ya dini, namna ya kuabudu, mifumo ya uendeshaji, uanachama au kuingilia uongozi wa Kanisa. Kanisa halipaswi kuomba nguvu au msaada wa kifedha kutoka serikalini ili kuendesha masuala ya kiroho. Huo ndio mfumo wa Kanisa la Agano Jipya.

Uhalisia wa injili na Kanisa hutambua huo uhusian. Biblia inasema watu wote waliumbwa na Mungu na kupewa upeo wa kumjua na kufuata kusudi lake (Mwanzo 1:27).kufuata kusudi la Mungu kunapaswa kuwa kwa hiari, sio kwa kulazimimshwa na Kanisa au na utawala wa nchi. Wokovu katika Kristo hutokana na uchaguzi wa hiari wa kumwamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi (Yohana 3:16; Waefeso 2:8-10). Hivyo, sio Kanisa wala nchi vinapaswa kuingilia uhuru wa kutangaza injili au uhuru wa watu kuikubali au kuikataa injili.

Kwa upande mwingine, Makanisa yanapaswa kuwa na watu ambao kwa hiari waliamua kubatizwa na kuwa washirika  (Matendo 2:41-42). Watu wanapewa wito wa kusaidia Makanisa kwa michango ya hiari kwa njia ya kutoa fungu la kumi na sadaka (2 Waefeso 8:1-15). Ni Yesu tu ndiyo Bwana, sio serikali wala taasis yeyote ya kidini (Waefeso 4:11-16; Wafilipi  2:8-11).

Historia ya mahusiano baina ya Kanisa-Serikali

Uthibitisho wa Kibiblia juu ya mahusiano baina ya Kanisa-Serikali ulitambuliwa.  Kwa miaka ya mwanzoni ya vuguvugu la Ukristo, Kanisa liliteswa kuttoka na serikali ya Kirumi. Kwenye karne ya nne, Serikali ya Kirumi iliamua kutolitesa tena Kanisa lakini pia kutoa nafasi kwa ajili ya kuendelea kwa Kanisa.

Huu uamuzi ulipelekea kuwa na umoja wa Kanisa na Serikali, huu umoja ulipelekea kuwa na Serikali yenye mfumo wa Kanisa. Mpangilio ulitofautiana karne kwa karne lakini jambo moja lilibaki kuendelea – kila hatu za kuendelea dini kasoro wenye ”msimamo maalum” walikuwa wakiteswa. Watu ambao walikuwa na imani ya uhuru wa Kanisa, mfano Wabaptist, walionekana kama waasi wa serikali na wasaliti wa uhusiano wa Kanisa-Serikali.

Nguvu ya kiserikali kwenye kuingilia masuala ya kidini ilisababisha ukuaji hafifu wa kiroho hivyo kuwa na serikali yenye Makanisa na idadi kubwa ya watu ambao hawakuwa na wokovu. Zaidi ya hapo, jitihada za kiserikali za kuzuia uanzishwaji wa dini ya kitaifa kulipokea vita ya wenyewe kwa wenyewe jambo ambali lilidhofisha tawala za serikali.  Hivyo, umoja wa Kanisa na Serikali ulikuwa nab ado ni hatarisha kwa pande zote mbili.

Wabaptist na Mahusiano baina ya Kanisa-Serikali

Wabaptist waliteswa vibaya mno kwenye mahusiano baina ya Kanisa na Serikali. Walifanya kampeni ya nguvu kudai uhuru wa dini, sio tu kwa ajiloi yao bali pia kwa ajili ya watu wengine. Nia yao ilikuwa kuwa na uhuru,sio tu kuachilia mambo yaendelee yalivyokuwa.

 Kumbukumbu za jitizada za Wabaptist kutaka uhuru wa kidini na utengani na serikali ni historia ya kutia moyo na kuiendeleza.  Kundi la watu wenye ushujaa waliendelea kushikilia imani zao licha ya kukabiliana na ugumu wa kutisha kutoka pande zote pindi watu wa dini na serikalini. Walifanya hayo kwa sababu waliamini kwamba walikuwa sahihi kwa mafundisho ya Biblia.

Kwa mfano, Thomas Helwys (1556-1616), Mchungaji wa Kibaptist huko London mwanzoni mwa miaka ya 1600, kwa uwazi alitangaza uhuru wa kidini. Huko Uingereza, Mfalme hakuwa tu kiongozi wa serikali lakini pia kiongozi wa Kanisa la Uingereza. Helwys alisisitiza kuwa Mfalme hakuwa na mamlaka juu ya masuala ya uhai wa masuala ya Kiroho. Alimtumia Mfamle nakala ya kitabu alichokiandika, “Mfalme ni mtu wa kawaida tu, sio Mungu.”

Mfalme  James alimweka Helwys gerezani,  na baadae akafariki kwa sababu ya msimamo wake wa kuisimamia imani.

Miaka michache baadae huko Marekani, Roger Williams (1603- 1683) alilasimishwa kuhama utawala wa Massachusetts Bay kwa sababu ya maoni yake ya kukubaliana na kutengana kwa  Kanisa na Serikali. Williams alianzisha yote mawili Kanisa la first Baptist  huko Marekani na utawala wa Kisiwa cha Rhode. Utawala huo ulifanikiwa kuwa na uhuru wa kidini moja kwa moja.  Aliandika kiapo,  “uzio au ukuta wa kutenganisha baina ya shamba la Kanisa na msitu wa ulimwenguni.”

Miaka ilipita, hata hivyo, kabla ya “ukuta wa utengano” kuwa msimamo wa nchi.  Wakati Katiba ya Marekani ilipelekwa mbele ya watu wenye kuipitisha haikuwa na kipengele cha uhuru wa kidini. Wabaptist waliungana na wengine kuwapinga wale waliokuwa wakitaka kuipitisha ili isipite hadi pale watakapoweka kipengele cha uhuru wa kidini. Hivyo basi, Marekebisho ya kwanza yalifanywa kwenye Katiba, kuelezea, “Baraza la bunge halitakuwa na mamlaka ya kutunga sheria juu ya uanzishwaji wa dini, au kuzuia uhuru wao wa namna yeyote, au kuzuia uhuru wa kuongea, wa kuhutubia, au uhuru wa watu waliokusanyika kwa amani, na kuishitaki serikali kwa kusababisha huzuni ya aina yeyote.”

Changamoto za kuwa na Kanisa huru na Nchi huru

Ugumu  wa utengano baina ya Kanisa na Serikali bado unaendelea. Maneno ambayo Truett alisema kwenye ngazi za ikulu  ya kutaka  “kuwa na mamlaka ya juu kila mahali ya kuwa na kanisa huru kwenye nchi huru”. Bado kufikiwa. Kwenye nchi zingine, umoja wa kidini na serikali vinaendelea, na kuna uhuru kidogo sana wa kidini au hakuna kabisa. Kwenye nchi zingine, hakuna kuchukuliana, hawana kabisa uhuru wa kidini, ni sheria tu ikifanya kazi. Bado kunamwendelezo wa kutumia fedha za walipa kodi ili kufadhili Makanisa na kusaidia uendeshaji wake.

Ili kuwa na matokeo mazuri kwenye huu utengani ndani ya dunia ambayo haitaki kubadilika ni changamoto kubwa. Kwa kutenganisha Kanisa na Serikali, Wabaptist hawana maana ya kusema ni kumtenganisha Mungu na Serikali. Wabaptist hawana jambo lingine tofauti kwenye huo uhusiano na wala hawautafsiri kinyume na tofauti.

Hata hiyo, Wabaptist wanaendelea kusisitiza kwamba sio Kanisa wala utawala wa Kiserikali kuingilia upande mwingine, kuonyesha mkazo kwamba Kanisa halipaswi kutegemea fedha na nguvu kutoka Serikalini ili kuendesha shughuli zake mbalimbali, na kuthibitisha kile kichoandikwa kihistoria kwamba Kanisa huru kwenye nchi huru kuna baraka pande zote.

Hitimisho

Nguvu za ndani ndio gharama ya uhuru, haswa uhuru wa kidini.  Wabaptist hivyo basi wana endelea kuzuia jitihada za kuingiliana kwa Kanisa na utawala wa nchi na kusisitiza utengano wa kiraffiki baina ya hizi pande pili huleta uhuru wa kidini.aptists,

“Kanisa na utawala wan chi vinapaswa kutengana…..
Kanisa huru kwenye nchi huru ni ukweli wa Ukristo….”
Imani ya Wabaptist