Wabaptisti:Kuwa na Ushirika wa Kanisa kwa kuzaliwa Upya ni Hatari?

“Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tama, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.”
Waefeso 5:5

Ubora wa kuwa muumini wa kanisa linasisitizwa kwenye imani ya Baptist. Wana-theolojia wa Baptist, Wachungaji na viongozi wengine kwa karne kadhaa wameamini kuwa hakuna mbadala wa kuzaliwa upya ndipo uwe mshirika wa Kanisa. Huo ndio ubora wake, lakini huo ndio uhalisia?

Kuna Ushahidi wa Kupinga juu ya Kuzaliwa Upya kama njia ya kuwa Mshirika wa Kanisa?

Mwanahistoria mashuhuri wa Baptist William R. Estep alisema, “Wabaptisti wa Marekani wako kwenye hatihati ya kupoteza hii maana ya kuzaliwa upya ndipo ufanyike kuwa mshirika wa Kanisa.”

Baadhi ya wachunguzi wa mwenendo wa Wabaptisti hukubaliana na Estep na kuwa ndio hitimisho lake kwa sababu kuna idadi kubwa ya wakaazi ambao sio washirika wa Kanisa la Baptist na hili linaonekana kwa sababu wakaazi wengi hawajishughulishi na masuala ya Kanisa, upungufu wa msaada wa fedha, uhafifu wa kujitoa kwenye uinjilisti, umisheni na kwenye huduma zingine, na aina ya maisha ambayo ni tofauti kabisa na mafundisho ya Yesu.

Ni kweli, baadhi ya hizo sababu zinatokana na hali tu zingine na sio kwa sababu ya hali ya kutozaliwa upya, kama “kugengeuka” au pengine kuwa “Mkristo mchanga” (1 Wakorintho 3:1-3; Waefeso 4:11-16). Kwa uhakika, kuna idadi kubwa ya washarika Makanisani ambao kiukweli ni wafuasi wa Kristo. Ila sidhani kama mambo kama hayo yangeshamiri kwa wingi endapo kungekuwepo waumini wa Makanisa ambao kweli kweli wameokoka.

Ni kwa nini dhana ya kuwa Muumini wa Kanisa mpaka Uzaliwe Upya kumepotea?

Japo hiyo hali ilikuweko kwa namna moja ama nyingine nyakati za Agano Jipya, ushahidi unaonyesha mambo haya yanazidi kushika kasi. Hakuna maelezo ya kina yaliyopo juu ya upotovu wa hii dhana ya kuzaliwa upya ili uwe mshirika wa Kanisa. Sababu hutofautiana kwa kanisa na Kanisa, zaidi ya hayo, sio Makanisa yote yaliyoathirika.

Sababu moja kubwa ya kushamiri huu mmomonyoko ni tabia mbovu zinazoendelea kuingilia tamaduni mbalimbali leo hii. Kwenye maisha ya Kanisa hili suala linaweza kutafsiriwa kuwa, “Sio jukumu langu kuhoji kama huyu mtu ameokolewa au hajaokolewa bali anakubaliwa tu kuwa mshirika wa Kanisa.”Matokeo yake, Kanisa linapokea watu ambao hawana uhakika nao juu ya wokovu na ushirika wa Kanisa. Wanasahau kwamba hilo suala la kujua hali ya Wokovu ni la umuhimu sana kuliko hata kuwa mshirika wa Kanis, bila kuficha linapaswa kuwa la kipaumbele kuliko suala la ushirika wa Kanisa. Mtu anaweza akawa anajua habari zote kuhusu Yesu na akawa na “majibu sahihi” juu ya wokovu (ufahamu wa kawaida tu) bila hata kuwahi kuwa na ushirika wa hii neema ya bure ya wokovu kwa kumwamini Kristo ( kusadiki kutoka moyoni.

Kupima nhali ya kiroho kwa wengine kunahitaji kuomba sana, kujishusha na kutafakari. Yesu alitoa angalizo juu ya kuwa hukumu wengine hali na sisi ni wenye dhambi (Mathayo 7:1-5; Yohana 8:1-11).  Kuwa Mfarisayo, mwenye ukali, kushika sana sheria za kuwa mtakatifu hakukufanyi kuwa Mkristo bora. Kwa maana nyingine, kushindwa kuishi kwenye mkazo wa Biblia na umuhimu wa ushirika wa kuzaliwa mara ya pili ni kukiuka mafundisho ya Kristo lakini pia kunapunguza utendaji wa Kristo (1 Wakorintho 5:9-13; Waefeso 5:1-7, 27; 2 Wathesalonike 3:14-15; Ufunuo 2:18-22

Hali ya jamii tuliyonayo huchochea kupunguzwa kasi kwa kusimamia ushirika kwa njia ya kuzaliwa upya. Kwa mfano, kwenye utandawazi wa mawasiliano na ongezeko kubwa la jamii kwenye miji kumesababisha kuwa na taarifa finyu juu ya mtu anayetaka kuwa mshirika wa Kanisa. Madhara yake, kumechanganya kwenye upande wa Kanisa kutokuwa na wasiwasi juu ya kuhukumu wengine, hivyo kutengeneza hali ya usawa na kuamini mtu ambaye hajaokolewa hawezi akaruhusiwa kuwa mshirika wa Kanisa.

Shinikizo la kuongezeko kwa washirika kanisani pia imekuwa sababu nyingine.  C. E. Colton aligundua jambo kutokana na hali ya kuwa kwenye Uchungaji kwa muda mrefu,  “Shinikizo  inayotumika kufanya uinjilisti kwa watu ambao wanachukuliwa kuwa ni wazuri kumechangia watu kujiunga na Kanisa bila kuokoka.”

Kubatizwa kwa watoto wadogo kwa baadhi ya Makanisa nayo ni sababu nyingine. Baadhi ya watoto wamekuwa wakibatizwa kwa nia mbaya; ni kweli kila mmoja anaweza. Lakini watoto inaonekana wanapendwa kubatizwa baada ya kuona watoto wenzao wamebatizwa au kwa sababu ya shinikizo kutoka kwa wazazi au kupitia waalimu wao wa shule ya Jumapili kubatizwa. Nin kweli, baadhi ya watoto wanaweza wakawa na uelewa wa kutosha wa kusema wanamhitaji Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao kwa sababu ya dhambi. Hivyo, wakiwa bado wadogo watoto hutaka kubatizwa, wanahitaji uangalizi wa karibu sana.

Huko nyuma Makanisa mengi ya Kibaptisti hawakukubaliana kabisa na mwenendo mbaya wa mshirika wa Kanisa kinyume na maisha ya Kristo. Endapo asingetubu, basi alikuwa anaondolewa kuwa mshirika wa Kanisa. Maandiko mbalimbali yametumika ili kukubaliana na uamuzi huo kama vile, Mathayo 18:15-20 na 1 Wakorintho 5:9-13. Makanisa ya leo hii yanaweka mkazo kwenye uinjilisti, mafundisho na kukua katika Kristo, wakisimamia maandiko haya Wagalatia 6:1, Waefeso 4:1-5:21 na yakobo 5:19-20. Lengo kuu kwenye hayo yote ni kufanya ushirika wa Kanisa uliozaliwa upya.

Ni kwa nini iwepo shida ya kutozingatia hali ya Kuzaliwa Upya ili uwe Mshirika?

Kupungua kwa hali ya kuzaliwa ndio uwe Mshirika wa Kanisa imekuwa ni shida kwa sababu mbalimbali.

Kukataa hilo fundisho muhimu la kuzaliwa upya ili uwe mshirika wa Kanisa kunaachilia hali ya kutothamini mamlaka ya Biblia.

Wabaptisti wanasisitiza kwamba Kanisa linapaswa kuwa na ushirika wa waumini makuhani. Ukuaji wa Ukristo husaidiwa pamoja na kuwa na shirika na waumini makuhani wengine. Endapo kanisa sio muunguniko wa waumini makuhani, huo ushirika hauwezi kuwa na maana iliyotarajiwa. Kiasi kwamba washiriki wote wataathirika.

Wabaptisti pia wanaamini kwamba Kristo ni Bwana sio tu kwa mmoja mmoja bali hata kwa Makanisa. Uongozi wa Kanisa la Baptisti unapaswa kuwa chini ya waumini ambao wako chini ya Mamlaka ya Kristo.  Kama washirika hawamtambui Kristo kama Bwana, maamuzi yote yanaweza kufanyika nje na kusudio la Kristo. Hii ina maana kwamba Kanisa litakuwa la anasa na la kidunia zaidi.

Kanisa la kidunia kama hilo halitakuwa na uweza wa kutimiza kusudi la Kanisa, kama vile uinjilisti, umisheni na huduma mbalimbali. Hivyo, ndio maana ni moja ya sababu mbalimbali ya kusisitiza ili Kanisa liendelee kuwepo.

Ni nini kifanyike cha ziada ili kufanikisha kuwa na Ushirika wa Kanisa kwa Kuzaliwa Upya?

Kupata kanisa ambalo lina watu ambao kweli kwa asilimia zote wamezaliwa upya ni changamoto. Hata hivyo, mengine yanaweza yakafanyika, kwa kufanya maombi kama nyenzo ya muhimu kwenye kila jambo linalofanyika.

Kanisa linapaswa kusisitiza kwenye suala la kuzaliwa upya ili kufanyika mshirika wa Kanisa, kusisitiza kwamba wokovu ni suala la muhimu na la kwanza kabla ya kuwa mshirika wa Kanisa. Kila mmoja aanze kuwajibika na kutathmini hali yake ya wokovu, kujibu maswali kama, “Ni kweli nimepata wokovu kwa njia ya imani kwa kumbali Kristo?” na “Ni kweli mimi ni Mkristo anayekua?” Watu wanapaswa kusisitizwa juu ya kutafuta ushauri wa kiroho endapo jibu ni “hapana”.

Kanisa linapaswa kuwa macho sana, kuwa na uhakika kwa njia ya upendo ili kutambua kwamba muumini anaetaka kujiunga ni kweli amezaliwa mara ya pili.

Kanisa pia linapaswa kuendelea na madarasa mbalimbali kwa ajili ya waumini watarajiwa na waumini wapya kwa kuwafundisha wokovu, umuhimu wa kuwa Mkristo mkomavu na matarajio ya kuwa mshirika wa Kanisa. Na hiyo darasa linapaswa kuwa na wale waumini wote ambao wamejiunga kwa njia ya barua au kwa kuja tu wenyewe.

Hitimisho

Tumadhamiria kufanya yote ambayo tunapaswa kuyafanya, kwa msaada wa Mungu, ili kuweza kupata kusudi la Biblia la kuwa na Kanisa lenye kuzaliwa upya. Kushindwa kufanya hivyo kutaleta madhara makubwa kwa watu, Kanisa na kuendeleza kile ambacho Kristo alichokianzisha.

“Wabaptisti wa Marekani wako kwenye hatihati ya kupoteza hii maana ya kuzaliwa upya ndipo ufanyike kuwa mshirika wa Kanisa.”
William R. Estep
Kwa nini Baptist?