Watumishi wawili wa Kanisa: Wachungaji na Mashemasi

“Paulo na Timotheo, watumwa wa Kristo, kwa watakatifu
wote katika Kristo Yesu

Walioko filipo, pamoja na Maaskofu na Mashemasi.”
Wafilipi 1:1

“Watumishi wa Kanisa la Agano Jipya ni Wachungaji na Mashemasi(Wafilipi. 1:1). Watumishi hao hao mara nyingine huitwa Askofu, mzee wa Kanisa au Mchungaji.”
Hershel H. Hobbs

Uadilifu wa Baptist kwa miaka yote wamethibitisha watumishi wawili walioandikwa kwenye Maandiko wa Kanisa la Agano Jipya, Mchungaji na Shemasi. Wabaptisti huamini kwamba Biblia inafundisha juu ya kila Mristo ameitwa kutumika na kuwahudumia wengine kwa jina la Kristo, lakini wengine wana wito maalum kama kipawa kutoka kwa Mungu ili kufanya majukumu maalum ndani ya huduma, kama mchungaji na shemasi.

Wachungaji wa Baptist

Wabaptist husadiki kwamba ofisi ya mchungaji ni moja kati ya ofisi mbili ambazo Kanisa zimeweka baada ya mfano kutoka kwenye Makanisa ya Agano Jipya. Biblia hutumia majina matatu ikimaanisha ofisi moja: Mzee, Mchungaji na Askofu. Kwa lugha ya Kigiriki ya Agano Jipya, haya majina huonyesha utofauti wa majukumu na sio kwamba ni watu tofauti (Matendo 20:17-28; 1 Petro 5:1-5).

Wabaptist hutumia Biblia ili kutambua sifa za mtu ambae anataka kuwa Mchungaji (1 Timotheo 3:1-7; Tito 1:5-9). Sifa zake kwa kawaida zimegawanywa kwenye sehemu mbili – tabia na vipawa vya huduma. Ofisi ya Mchungaji inapaswa kutumika ili kuwatumikia wengine, sio kwa ubinafsi au kwa namna ya kujiinua.

Kila Kanisa la Kibaptist huchagua (kumwita) yule ambayo wao wanaona anafaa kuwa Mchungaji wao. Hatua za kufanya hivyo huwa hutofautiana kwa mbali baina ya Makanisa., lakini hatua zifuatazo zinafuata na wengi wao.

  • Kama Kanisa halina kabisa Mchungaji ushirika unaunda kamati maalum ya kutafuta Mchungaji kwa maombi huku wakiendelea kuchambua sifa za watu mbalimbali ambao hudhani wanaweza kufaa.
  • Baada ya majadiliano ya kina, kamati hupendekeza jina la mtu kwa Kanisa ambaye wanaamini Mungu amemkubali kuwa Mchungaji.
  • Mchungaji mtarajiwa analitembelea Kanisa husika na kuhubiri kwa “mwaliko maalum” ili kuona kipawa chake. Baada ya hapo Kanisa linapiga kura za ndio au hapana. Kama kura zimekuwa nyingi za ndio, Mchungaji mtarajiwa kwa nafasi yake pia anaweza akakubali au akakataa.
  • Mchungaji anaweza akaendelea kutumika na ushirika wa mahali endapo mahusiano ya pande zote mbili yako vizuri na wamekubaliana kuendelea.

Uhusiano baina ya Mchungaji na kanisa ni wa maana sana. Kila mmoja anayo nafasi na wajibu endapo, yakiwa sawa bila shida, basi uhusiano huwa wenye faida na kuzaa matunda. Kwa mfano, Kanisa linapaswa kuwa la maombi, kusaidia kwa kwenye eneo la uchumi, kumtia moyo na kumsaidia Mchungaji ili utendaji wake ndani ya Kanisa uwe mzuri. Pia kwa upande mwingine, Mchungaji anapaswa kuwa wa maombi, kutoa huduma, na kufundisha na kuwa na uongozi wa Kimungu kwa washirika wa Kanisa.

Mashemasi wa Baptist 

Ofisi ya pili ndani ya Kanisa la Baptist ni Shemasi. Wakati Wachungaji huchaguliwa watu walio nje na ushirika wa Kanisa, Mashemasi huchaguliwa miongoni mwa waumini wa Kanisa. Sifa za Mashemasi Kibiblia (1 Timotheo 3:8-13) hutazamwa sana kwenye tabia na mahusiano yake ndani ya Kanisa, familia na jamii. Mashemasi wanapaswa kuwa watu wasio na hatia na wenye imani thabiti na kumtegemea Roho Mtakatifu.

Matendo ya Mitume 6:1-6 tunasoma kuanzishwa kwa huduma ya Mashemasi. Wanapaswa kutoa msaada wa mahitaji ya kimwili ili Wachungaji waendelee kushughulikia mahitaji ya masuala ya Kiroho. Mashemasi wasichukuliwe kama baraza la uongozi wa Kanisa bali kama viongozi watumwa.

Kwenye Kanisa la Baptist suala la kupata Mashemasi huhusisha washirika wote wa Kanisa. Japo Makanisa hutofautiana haswa kwenye hatua mbalimbali za kufuata, japo la msingi ni ushiriki wa waumini kwenye upigaji kura na kuamua nani wanafaa kuwa Mashemasi.

Wajibu wa Shemasi hutofautiana Kanisa kwa Kanisa. Kwenye Makanisa mengi, Mashemasi wana jukumu la kutathmini na kupitisha masuala makubwa ambayo huletwa mbele ya Kanisa nzima kwa ajili ya uamuzi wa kura. Makanisa huhusisha Mashemasi kwenye maeneo mablimbali ya huduma, kama vile kutembelea wagonjwa, kusaidia familia zilizoingia kwenye shida na hata kutoa msaada kwa watu masikini.

Suala la Kuwekwa Wakfu kwa Wabaptist 

Wabaptisti huamini kwamba suala la kuwekwa wakfu halimpi mtu nguvu zaidi wala mamlaka. Bali ni njia nya kuonyesha kwa Makanisa na ulimwengu kwamba mhusika anafaa na anakidhi kuwa Mchungaji au Shemasi. Kwa miaka ya hivi karibuni, Wabaptist wameendelea mbele zaidi na suala la kuwekwa wakfu kiasi cha kwamba kuwafanyia wengine wanaoingia kwenye huduma, kama vile, viongozi wa dini, wamisheni na wahudumu wa Kanisa.

Sio Wabaptisti wote wanaokubaliana kwamba kuwekwa wakfu ni muhimu na hata kama kuna haja. Hata hivyo, suala la kuwekwa wafku hufanywa na Makanisa mengi ya Kibaptisti na kwa kadri muda unavyoendelea huonekana kuwa ni jambo linalokubalika. Hivyo, mtu anapohama kutoka Kanisa lingine kama Mchungaji au Shemasi, hakuna haja ya kuwekwa tena wakfu.

Kwa Wabaptisti, kuwekwa wakfu ni shughuli ya Kanisa husika, na sio dhehebu. Japo Makanisa mengine na hata viongozi mbalimbali wa dini wanaweza kualikwa kuhudhuria, Kanisa ndio lenye mamlaka ya kuweka wakfu

Kwa upande wa Wachungaji, kuwekwa wakfu hufuata zoezi la kupewa leseni ya kuonyesha sasa huyo mtu ni Mchungaji na anapaswa kufanya huduma mbalimbali za Kiinjili. Wahusika wa kutoa leseni (kibali) hutoa muda fulani wakati Kanisa na wahusika hufanya tathmini endapo mhusika anafaa kwa huduma ya Uchungaji. Kama mhusika amethibitisha kwa wito wa ndani kwamba ameitwa na Mungu kupitia Roho Mtakatifu kwa ajili ya huduma ya Injili, hushuhudiwa pia na sifa za Kibiblia kwa ajili ya hiyo huduma na jinsi vipawa vyake vinavyotumika kwa ufanisi bora wa huduma ya Kichungaji, Kanisa linaendelea na utaratibu wa kuwekwa wakfu.

Upekee wa Baptist Huhusiana na Wachungaji na Mashemasi

Uadilifu wa Baptist juu ya Wachungaji na Mashemasi huhusiana kwa ukaribu na upekee wa Wabaptisti. Kwa mfano, Biblia ndiyo yenye mamlaka juu ya imani na desturi za Wabaptisti. Wabaptisti hutafsiri Biblia kama inavyoeleza juu ya uwepo wa ofisi mbili kwenye Kanisa la Agano Jipya – Mchungaji na Shemasi.

Biblia inafundisha kwamba watu wote waliomwamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi hufanyika kuwa Makuhani wakiwa na uwezo wa kuwasiliana na Mungu moja kwa moja (1 Petro 2:5; Ufunuo 1:6; 5:10). Hakuna haja ya kuwa na darasa maalum la kikuhani (Waebrania 8 – 10). Hivyo, Wabaptisti hawatumii neno “kuhani” wakimaanisha Mchungaji au kwamba Mchungaji hufanya majukumu ya kikuhani, akiwa kama msemaji wao baina yao na Mungu.

Wabaptisti huamini dhana ya Kibiblia juu ya ukuhani wa waumini na uweza wa roho na sio kwa maana ya kushusha hadhi na majukumu ya Mchungaji. Wakati waumini makuhani wote ni sawa, wengine waliitwa na Mungu na kuchaguliwa na washirika wa Kanisa kuwa Wachungaji-Viongozi. Waumini hawapaswi kuwakata Wachungaji na wajibu wao wa kulisoma na kuitafsiri Bibli na kutimiza kusudi la Kristo na kumfuata yeye kama Bwana wa milele.

Wabaptisti huamini kwenye uongozi shirikishi na dhana ya kujitegemea kwa Makanisa. Hivyo basi, Wachungaji hawachaguliwi na chombo kingine nje ya ushirika wa Kanisa la mahali. Kila Kanisa linao wajibu wa kumtafuta Mchungaji na hata kuchagua Mashemasi. Uongozi uko mikononi mwa Kanisa nzima, na sio Mchungaji wala Shemasi. Biblia inasema Mchungaji anapaswa kuonyesha uongozi thabiti na wenye nguvu, na sio uongozi wa mabavu I1 Petro 5:1-5).

Uhuru na kujitegemea kumefanya kuondoa tofauti ndani ya maisha ya Waabaptisti. Hili limetokana na suala la Wachungaji na Mashemasi. Kwa mfano, kupitia historia ya Wabaptisti, Makanisa yalitaka mtu apitie kwenye nafasi mbalimbali kabla ya kuwa Mchungaji. Wabaptisti pia hutofautiana kama ni sawa wote wanaume na wanawake kuwa Wachungaji au Mashemasi. Idadi, mahitaji na kazi za Mashemasi hutegemea Kanisa kwa Kanisa

Hitimisho  

Japo kuwa tofauti zipo miongoni mwa Wabaptisti kuhusiana na suala la ofisi mbili za Uchungaji na Mashemasi, Wabaptisti wanakubali kwamba Mungu aliweka hizi nafasi mbili ili kufanya viongozi kuwa watumwa ndani ya Kanisa.