Wabaptisti: Nani? Nini? Kwa nini? Wapi? Lini?

“Naam, nimepata urithi mzuri.”
Zaburi 16:6

“Kila Mbaptisti anapaswa kujitambua kwa nini anaitwa Mbaptisti,na kwa kutambua kutokana na ukweli ulioko kwenye Neno la Mungu. kwa kulitambua hilo hakuna maana ya kuliudhi Kanisa kwa namna moja ama nyingine.”
George W. Truett
Mchungaji wa Kanisa la First Baptist kutoka  Dallas, 1897-1944

Idadi ya Wabaptisti ulimwenguni ni kubwa sana na mara nyingi husikika habari zao. Lakini yapo mambo machache ambayo dunia hujua kuhusu Wabaptisti na kwa kawaida mengine ni kushindwa kuwaelewa vizuri Wabaptisti. Hata pia baadhi ya Wabaptist wenyewe hawajui vizuri juu ya Imani na destruri, urithi na historia.

Mfano,  uliwahi kujua…

…Mchungaji wa Baptist alikuwa wa kwanza kuunda serikali ya kwanza ya Marekani iliyotoa fursa ya uhuru wa kuabudu kwa wote.

…Wamisheni wa kwanza wa Baptist kutoka Marekani hawakuwa Wabaptisti lakini wakati wakisafiri kwenda kwenye eneo la Umisheni wakafanyika kuwa Wabaptisti.

…Mchungaji wa kwanza wa Baptist huko Uingereza alifungwa gerezani na 1 Mfalme James (Mwasisi wa toleo la Biblia aina ya King James) kwa sababu alikuwa akisisitiza uhuru wa kuabudu kwa kila mmoja.

…Rais wa kwanza Mteule wa Jamhuri ya Texas alifanyika kuwa Mlei wa kuigwa ndani ya Wabaptisti wa Texas.

…Wabaptisti wa kwanza waliweza kubatiza kwa maji machache na sio kwa kuzamishwa lakini baada ya muda wakatambua kwamba ubatizo ulio sahihi kwenye Biblia ni wakuzamisha kwenye maji.

…Wabaptisti wa kwanza kule Marekani walicharazwa viboko mbele ya umati wa watu kwa kosa la kuimba wakati wa ibada kwa sababu wengine walidhani kufanya hivyo sio kiroho na kibiblia.

……Mmisheni wa kwanza wa Kibaptisti kutoka Marekani kwenda nchi nyingine alikuwa ni Mmarekani-Mweusi ambaye awali alikuwa ni mtumwa.

… Mchungaji wa Baptist kutoka Texas alihubiri kwenye Ikulu ya Marekani Washington D.C kwenye siku ya uhuru wa kuabudu.

…Mchungaji wa Kibaptisti kutoka Virginia alikutana na James Madison akiwa na lengo la kumtia moyo juu ya marekebisho ya katiba ya nchi ya Marekani ambayo yalilenga kutoa uhuru wa kuabudu.

…Mwinjilisti maarufu duniani na anaefahamika ulimwenguni kote ni Mbaptisti ambaye alianza katikati ya karne ya Ishilini.

…Mtu wa kwanza kupata ubatizo kwenye Ghuba ya Mexico akiwa Mbaptisti wakati Jimbo la Texas lilikuwa taifa linalojitegemea na kuwa la kwanza kujenga kiwanda cha kusindika maziwa.

…Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Watu wa Marekani na mshindi wa tuzo ya Utakatifu ni Mtaua Mbaptisti na Mwalimu wa Shule ya Jumapili.

…kwamba Mfanyabiashara mkarimu ambaye alikuwa Mbaptisti alikuwa mtu wa kwanza kusindika siagi.

…kwamba Mwandishi wa kitabu maarufu cha kuabudu kinachoitwa “ Uliye Juu ni wewe pekee” alikuwa Mbaptisti aliyetoka kwenye familia ya kumcha Mungu, baba yake na kaka yake walikuwa Wachungaji wa Baptisti.

Hizi  “uliwahi kujua” ni habari za kufurahisha mno (tutapata habari nyingi zinanohusiana na hizo kwenye mwendelezo wa hizi makala) lakini hazionyeshi bayana kwamba ni imani zipi na destruri ambazo huachilia kuwa ni Wabaptisti. Kama mwingine angekuuliza swali, “Ni kitu gani kimoja ambacho kinatofautisha Wabaptisti na Wakristo wa madhehebu mengine?” jibu lake ungejibuje? Au pengine ukauliuzwa, “Ni tofauti ipi inayokufanya kuwa Mkristo wa Kibaptisti?” ungesema nini? Kwenye wiki zijazo tunapoendelea na mfululizo wa hizi makala tutajifunza juu ya hayo maswali.

Kwa nini kuna Upungufu wa Uelewa juu ya Wabaptisti?

Kwa nini Wabaptisti wengi siku hizi wanashindwa kujua nini maana ya kuwa Mbaptisti? Kuna sababu nyingi ambazo zimepelekea kufikia hapa tulipo kwa nini kuna upungufu wa uelewa:

* Uundwaji wa Idara mbalimbali za kujifunza kwenye Makanisa (japo kila eneo hutofautiana lakini lengo kuwa ni “kuwafanya kuwa wanafunzi”) zililenga kusisitiza juu ya mafundisho ya Kibaptisti, desturi, na historia, lakini kwa sasa mikazo hiyo haipo tena.

* Asilimia kubwa ya watu wamejiunga na Kanisa la Baptist hivi karibuni kutoka kwenye madhehebu mengine , baadhi yao wamejiunga wakiwa na ufahamu mdogo sana na wengine hawana kabisa ufahamu wa msingi wa Kanisa. Kwa sababu zote hizo mbili ufahamu wao juu ya Imani na destruri za Wabaptisti ni mdogo mno.

* Japo yapo baadhi ya Makanisa isipokuwa sio yote, kiasi fulani husaidia kuelimisha waumini kuelewa nini ya kuwa mshirika wa Baptist na kwa nini liitwe Kanisa la Baptist

*Japo watu wengine huamini kuwa suala la madhehebu ni jambo la nyuma sana na halina umuhimu wowote kwa sasa. (Ukweli ni kwamba dhehebu la Baptist linakuwa, halififii, na utofauti wa madhehebu ni jambo la umuhimu wake pia kulielewa)

Nia ya kukuza mafundisho ya Baptist

Huo uhaba wa kuelewa kwamba Wabaptisti wakoje, kwa Wabaptisti wenyewe na wale wasio Wabaptisti, kumepelekea mwanga sasa wa kuamsha nia na kiu ya kujua mafundisho, destruri na urithi wetu kama familia ya Wakristo wa Kibaptisti.

Tunatambua mchango wa maana ambao George W. Truett, Mchungaji aliyejizolea umaarufu wa Kanisa la First Baptist huko Dallas, alioutoa kwenye karne iliyopita. “Kila Mbaptisti anapaswa kujitambua kwa nini anaitwa Mbaptisti,na kwa kutambua kutokana na ukweli ulioko kwenye Neno la Mungu. kwa kulitambua hilo hakuna maana ya kuliudhi Kanisa kwa namna moja ama nyingine.”

Wabaptisti wa zamani walishika saana hayo mafundisho na destruri za Wabaptisti kitendo ambacho kilifanya kuimarika kwa dhehebu. Walifanya hayo, sio kwa nia ya kuonekana kuwa watu wa upeke fulani, bali ni kwa sababu walijengwa kwenye uthibitisho wa Neno la Mungu. walivumilia mateso mbalimbali yakiwemo kutoka kwenye mamlaka ya Kiserikali na hata makundi mengine ya Kikristo. Walifanyiwa kejeli, kutozwa faini mbalimbali, kupigwa mbele ya umati wa watu, kufungwa jela na wengine hata kufa kwa sababu ya kulisimamia kweli Neno la Mungu. kiukweli hatuhitaji kulifanyia mzaha hili suala, tunahitaji hata kuchukua hatua za ziada kwa ajili ya kizazi kinachokuja ili kuisimamia imani yenye msingi wa Kibiblia na kwamba wengine walijitoa kwa gharama zote na kuweza kuutunza hadi kufikia hapa tulipo.

Kipekee, tushukuru kwa msisitizo mpya juu ya mafundisho ya Kibaptisti, desturi na urithi unaendelea kuchochewa kwa upya. Mwaka 1994, Jumuiya Kuu ya Jamhuri ya Texas iliunda vitengo maalum viwili vyenye kuhabarisha na kuchochea watu kujua juu ya mafundisho na heshima yaa Wabaptisti. Vyuo vya Kibaptisti hutoa masomo mbalimbali ya kumtambulisha Mbaptisti. Asilimia kubwa ya Makanisa pia hufanya warsha na makongamano yenye mafundisho ya Kibaptisti. Vitabu na makabrasha mbalimbali juu ya mafundisho ya Kibaptisti na urithi wao vinaendelea kuchapishwa. Wachungaji wengi pia wanaendelea kuhubiri mahubiri yenye uthamani wa kuwa Mbaptisti.

Mfululizo wa makala mbalimbali kwa mwaka mzima juu ya umuhimu wa mafundisho ya Kibaptisti

Bwana Noble Hurley alionyesha kiu ya kusaidia hili eneo la kuelezea ukweli wa Baptist na jinsi walivyo ili kuchochea watu kuendelea kutamani kuwa Wabaptisti na kutoa upotoshwaji uliopo na ufahamu mdogo juu ya Wabaptisti. Hivyo, kabla ya kifo chake mnamo mwaka 2004, alitoa mahitaji mbalimbali kwa ajili ya hiyo kazi. Huu mfululizo wa makala hizi kwa mwaka mzima ni kutokana na ukarimu wake.

Hizi makala sio makala rasmi juu ya mafundisho ya Kibaptisti. Ukweli, hakuna ukiri “rasmi” wa namna hiyo ambao uliwahi kuwako. Hakuna msemaji Mbaptisti awezae kusema kwa niaba ya Wabaptisti wote. Hivyo basi haya masomo/makala ni mtazamo wa Mbaptisti mmoja tu, mwandishi.

Huu mfululizo wa masomo utajikita zaidi kwenye misingi ya Wabaptisti na destruri, kwa kubainisha ukweli wa Kibiblia na historia. Mada zilizomo ni pamoja na Uungu wa Kristo, Mamlaka ya Biblia, Uwezo wa roho, Wokovu, Ukuhani wa Muumini, Ubatizo wa muumini, Ushirika na heshima, uhuru, Uhiari wa kujitoa, Uhuru wa kuabudu na kujitenga kwa Kanisa na serikali, na masuala ambayo Baptist hulinganishwa na ulimwengu.

Baadhi, kama sio asilimia kubwa ya hizi mada zinaushindani ndani yake. Hilo sio jambo la ajabu. Kutofautiana mawazo kwa Wabaptisti si jambo jipya. Imewahi kusemwa kuwa Wabaptisti sio watu wa kunyamaza, bali Wabaptisti ni watu wanaopenda kutoa uhuru wa maoni yao ili kuonyesha kile walichokiamini. Uhuru wa kujieleza na kutoa maoni yetu ndicho kinachotufanya tuwe tofauti.

Ni kweli, sio masomo yote ya hizi makala zimejitosheleza kuelezea kila kitu, ili kuhakikisha kuwa taarifa nyingi zinapatikana, kuna tovuti ambayo itakusanya karibia kila makala na maelezo zaidi. Angalia www.baptistdistinctives.org.

Hizi makala huambatana na maombi kiasi cha kwamba baada ya kumaliza sio tu kwamba utapata uelewa wa nani, nini, kwa nini, wapi na lini kuhusu Wabaptisti bali kumweneza Kristo ulimwenguni kote.

Kwa taarifa zaidi tembelea  www.baptistdistinctives.org.

Kutimiza nia ya kuelezea upekee wa Wabaptisti, Noble Hurley, muda mfupi kabla ya kifo chake 2004, alianzisha mfuko maalum kwa jina la Jane and Noble Hurley Baptist Identity Fund wenye lengo la kutoa haya mafundisho na alimwomba William M. Pinson Jr. and Doris A. Tinker kuandaa hizi makala (Makala 1)
_ _ _ _ _ _ _ _

MAJIBU YA SEHEMU YA ULIWAHI KUJUA YA MAKALA HII

…Mchungaji wa Baptist alikuwa wa kwanza kuunda serikali ya kwanza ya Marekani iliyotoa fursa ya uhuru wa kuabudu kwa wote.
ROGER WILLIAMS

…Wamisheni wa kwanza wa Baptist kutoka Marekani hawakuwa Wabaptisti lakini wakati wakisafiri kwenda kwenye eneo la Umisheni wakafanyika kuwa Wabaptisti.
ADONIRAM AND ANN HASSELTINE JUDSON

…Mchungaji wa kwanza wa Baptist huko Uingereza alifungwa gerezani na 1 Mfalme James (Mwasisi wa toleo la Biblia aina ya King James) kwa sababu alikuwa akisisitiza uhuru wa kuabudu kwa kila mmoja.
THOMAS HELWYS

…Rais wa kwanza Mteule wa Jamhuri ya Texas alifanyika kuwa Mlei wa kuigwa ndani ya Wabaptisti wa Texas.
SAM HOUSTON

…Wabaptisti wa kwanza waliweza kubatiza kwa maji machache na sio kwa kuzamishwa lakini baada ya muda wakatambua kwamba ubatizo ulio sahihi kwenye Biblia ni wakuzamisha kwenye maji.
EARLY GENERAL BAPTISTS

…Wabaptisti wa kwanza kule Marekani walicharazwa viboko mbele ya umati wa watu kwa kosa la kuimba wakati wa ibada kwa sababu wengine walidhani kufanya hivyo sio kiroho na kibiblia.
BAPTISTS IN COLONIAL AMERICA

……Mmisheni wa kwanza wa Kibaptisti kutoka Marekani kwenda nchi nyingine alikuwa ni Mmarekani-Mweusi ambaye awali alikuwa ni mtumwa.
GEORGE LIELE

… Mchungaji wa Baptist kutoka Texas alihubiri kwenye Ikulu ya Marekani Washington D.C kwenye siku ya uhuru wa kuabudu.
GEORGE W. TRUETT

…Mchungaji wa Kibaptisti kutoka Virginia alikutana na James Madison akiwa na lengo la kumtia moyo juu ya marekebisho ya katiba ya nchi ya Marekani ambayo yalilenga kutoa uhuru wa kuabudu.
JOHN LELAND

…Mwinjilisti maarufu duniani na anaefahamika ulimwenguni kote ni Mbaptisti ambaye alianza katikati ya karne ya Ishilini.
BILLY GRAHAM

…Mtu wa kwanza kupata ubatizo kwenye Ghuba ya Mexico akiwa Mbaptisti wakati Jimbo la Texas lilikuwa taifa linalojitegemea na kuwa la kwanza kujenga kiwanda cha kusindika maziwa.
GAIL BORDEN JR.

…Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Watu wa Marekani na mshindi wa tuzo ya Utakatifu ni Mtaua Mbaptisti na Mwalimu wa Shule ya Jumapili.
JIMMY CARTER

…kwamba Mfanyabiashara mkarimu ambaye alikuwa Mbaptisti alikuwa mtu wa kwanza kusindika siagi.
JAMES L. KRAFT

…kwamba Mwandishi wa kitabu maarufu cha kuabudu kinachoitwa “ Uliye Juu ni wewe pekee” alikuwa Mbaptisti aliyetoka kwenye familia ya kumcha Mungu, baba yake na kaka yake walikuwa Wachungaji wa Baptisti.
OSWALD CHAMBERS