Wokovu ni kwa Neema kwa Njia

“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.”
Waefeso 2:8-9

Mazungumzo ya kawaida, tamthilia, vipindi vya kwenye luninga, katuni za vichekesho vyote hivi kuonyesha kwamba dhana ya wokovu ni kwamba: Mtu akifa, Mungu anapima matendo yake mema na mabaya. Kama matendo mema yakiwa yamezidi kuliko mabaya, basi huyo mtu moja kwa moja anaenda mbinguni. Ila kama matendo mabaya yamezidi matendo mema basi huyo mtu anaenda jehanamu. (wakati mwingine hata uhalisia kwa jehanamu hauonyeshi kwa mfumo wa picha.) Kwa maneno mengine, matendo ya mtu hutoa njia ya kwenda mbinguni au jehenamu.

Msimamo wa Biblia juu ya wokovu ni tofauti kabisa na hiyo dhana. Biblia inafundisha wazi kwamba watu wote wametenda dhambi  (Warumi 3:23) na mshahara wa dhambi ni mauti. Hata hivyo, Mungu kwa neema yake ametoa njia ya kuweza kusamehewa dhambi, kitendo kinachopelekea  kuikosa jehanamu na kuipata mbingu. Hiyo njia ni kumwamini Mwanae, Yesu Kristo (Warumi 6:23).

Wokovu , kulingana na Biblia, ni kwa neema kwa njia ya imani, sio kwa kufanya matendo mema la hasha (Waefeso 2:8-9). Ni kweli tunakubaliana na kufanya matendo mema, kwa wakati wote kulingana na historia ya Wabaptisti wamekuwa wakifundisha na kuamini kuwa wokovu ni kwa neema kwa njia ya imani tu.

Neema/Kwa njia ya Imani kupata Wokovu

Wabaptisti huamini kwamba wanadamu wote walichagua kutenda dhambi, kwa maana ya kusema, kutomtii Mungu. Madhara ya dhambi ni kifo. Wanadamu hawana uwezo wa kujiokoa wenyewe kutoka kwenye hili janga, Mungu, kwa sababu ya upendo wake kwa wanadamu, ametoa wokovu (Yohana 3:16).

Zawadi ya Mungu ya wokovu kwetu hupatikana kwa njia ya imani kupitia Mwanae, Bwana Yesu Kristo. Kwa kujitoa uhai wake, kwa kufa msalabani, Yesu alitoa njia ya kutoka wafu na kuingia uzima wa milele. Hiyo njia ni uthibitisho wa hii neema ya Mungu. hii njia hupatikana kwa imani tu (Warumi 5:1-2).

Japo Biblia huelezea mifano mbalimbali ya kuonyesha ni jinsi gani Yesu alionyesha njia ya wokovu kwa wanadamu waliopotea, kwa kila mfano yake kila kitu kipo wazi: Wokovu hupatikana kwa njia ya kumwamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi. Madhehebu mengine yameongeza baadhi ya mambo kama hatua za kupata wokovu nazo ni pamoja na ubatizo, ushirika wa kanisa, matendo mema na sakramenti. Wabaptisti wanafundisha na kuamini kwamba wokovu ni kwa njia ya kumwamini Yesu ambaye alitolewa kwetu kama thawabu kwa neema yake Mungu.

Wokovu ni Bure lakini ni Gharama pia

Wakati Baptist hukiri  ya kwamba wokovu hupatikana bure, kama thawabu kutoka kwa Mungu, lakini pia wanakiri kwamba ni gharama. Wokovu ulimgharimu Mungu kifo cha Mwanae mpendwa. Wokovu ulimgharimu Yesu kudhihakiwa, kuteswa na hata kutundikwa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu. Katika kuufikisha ujumbe wa wokovu kwa karne na karne kumeweza kuwafanya Watakatifu Waaminifu kuteswa, kufungwa jela na hata kufa pia. Wokovu pia ni gharama kwa ambaye kwa njia ya imani anaipokea hii thawabu ya neema kutoka kwa Mungu, humgharimu kuachana na maisha yake ya zamani, yaani anakuwa amekufa kwayo (Mathayo 16:24-25).

Hivyo basi, wokovu usichukuliwe kama ni jambo jepesi jepesi. Kuzungumzia suala la wokovu juu juu ni kukataa ukweli wake. Wabaptisti huamini kwamba umilele wa kila mwanadamu hutegemea imani aliyonayo juu ya Yesu ambaye ni thawabu kwetu kwa neema yake Mungu. Kwa msingi huo, Wabaptisti wamejitoa kwa ajili ya kufanya uinjilisti na umisheni.

Wokovu ni hatua ya Neema kwa njia ya Imani

Kwa matendo kauli za wabaptisti huonyesha kuamini na kusisitiza kwamba Biblia hufundisha kuwa wokovu ni pamoja na “kuzaliwa upya” (wengine kusema “uhalali”), “kutakaswa” na “kutukuzwa”. Wabaptisti wengine huelezea hivi: tumeokolewa kutoka kwenye adhabu ya dhambi (kuzaliwa upya), tunaokolewa kutoka kwenye nguvu ya dhambi (kutakaswa) na tutaokolewa kutoka kwenye uwepo wa dhambi (kutukuzwa), au wengine hufupisha kwa kusema: tumeokolewa, tunaokolewa na tutaokolewa.

Lakini ukweli unawekwa wazi,  msisitizo unabaki kuwa ni kwa neema kwa njia ya imani. Neema ya Mungu sio tu humfanya mtu kuanza safari ya Ukristo bali pia kumalizia safari. Njia ya wokovu huenda kwa imani (Wagalatia 2:16-20).

Hatua ya wokovu huleta mabadiliko kwenye maisha, sio tu kwamba baada ya hapa tulipo, lakini kuanzia hapa na hata sasa. Matendo mema hayatufanyi kupata wokovu, lakini wokovu unatakiwa uonyeshe matendo mema. (Waefeso 2:10)

Imani ya kweli hailazimishwi

Wabaptisti husisitiza kwamba kamwe isiwepo nguvu ya ziada ya kutumika ili kumfanya mtu amwamini Yesu na kuupata wokovu. Ni dhahiri, Wabaptisti huamini kwamba imani ya kweli sio ile ya lazima. Imani ya kweli ni ile ya uhiari.

Wabaptisti wanatambua kuwa kamwe Yesu hakuwahi kumlazimisha mtu amfuate. Huduma ya Yesu inaonyesha kwamba watu walikuwa na uwezo wa kumwamini au kumkataa. Japo Yesu aliweka wazi  madhara ya kuamini na kutokuamini, hakuweza kutumia nguvu ya aina yeyote ili kuwafanya watu wamfuate Yeye. Zaidi ya hayo, Wanafunzi wake Yesu walionyesha imani yao kwa uhiari kwa kuipokea injili.

Hivyo basi, Wabaptisti wanasisitiza kamwe asiwepo mtu wakulazimisha ili kumwamini Yesu. Kama George W. Truett alivyozingatia, “Mateso yanaweza kumfanya mtu kuwa mnafiki, lakini hayawezi kuwafanya kuwa Wakristo.” Wakati wote Wabaptisti wamekuwa wakisisitiza uhuru wa kuchagua – kwa kumaanisha, uhuru wa kuabudu.

Neema/Imani na Enzi kuu ya Mungu/Uhiari wa Mwanadamu

Wakati Wabaptisti husadiki juu ya Mafundisho ya Biblia kwamba wokovu ni kwa neema ka njia ya imani tu, wametofautiana uhusiano wa neema na imani kwenye wokovu. Kwa mfano, sio Wabaptisti wote wanakubaliana na uhsuiano ulipo kati ya Enzi Kuu ya Mungu na uhiari wa Mwanadamu.

Wabaptisti wengine wamesisitiza suala la Enzi kuu ya Mungu na kusadiki kwamba ni wale tu ambao tangu zamani Mungu aliwachagua ndio wataokolewa kwa imani, husisitiza kwamba wokovu huu hauwezi kupotea. Wabaptisti wengine husisitiza kwamba uhiari wa Mwanadamu na kusadiki kwamba wale wote ambao wataitikia kwa imani zawadi ya neema ya Mungu wataokolewa; wengine huamini kuwa wokovu wa namna hii unaweza ukapotea.

Wabaptisti wengine huamini kwamba Biblia iliweka mambo yote pamoja yaani Enzi kuu ya Mungu na uhiari wa Mwanadamu wa kuchagua. Japo kweli hizi mbili zinaonekana kutopatana na utashi wa Mwanadamu, Wabaptisti husadiki zote kwa pamoja na mara nyingi sio kwa kutumia nguvu ya ziada ili kuzipatanisha. Kama wabaptisti walioandika Makala juu ya Imani kwa ajili ya Umoja wa Wabaptisti Washirika mnamo mwaka 1840 walisema, “Tunaamini kwenye mafundisho ya Enzi kuu ya Mungu, na uhiari wa Mwanadamu na uwajibikaji wake.” Pia walisema, Tunaamini kwenye mateso ya mwisho ya watakatifu kwa neema mpaka kwenye utukufu.”

Ndio maana Wabaptisti wengi wanaweka mkazo kwamba kila mtu anao uhiari wa kuchagua kumwamini Kristo kama Bwana na Mwokozi wake au kumkataa Kristo. Pia husisitiza kuwa kila mmoja anayekubali kwa njia ya kutubu juu ya uhai wa Yesu, kifo na ufufuo ataokolewa (1 Timotheo 2:3-4; 2 Petro 3:9; 1 Yohana 2:2). Kwa uthibitisho zaidi walinukuu maneno ya Yesu, “Ili kila mtu aaminiye asipotee, awe na uzima katika Yeye” (Yohana 3:15). Huamini pia kwamba mtu akishaokolewa kweli kweli, anakuwa chini ya ulinzi wa nguvu za Mungu, jambo ambalo linaweza kusemwa kuwa ni ulinzi kwa aliyeamini (Yohana 10:27-30).

Hitimisho

Japo sio Wabaptisti wote hukubaliana na maana halisi ya neema na imani, lakini Wabaptisti wote hukubaliana kwamba wokovu ni kwa neema ya Mungu kwa njia ya imani. Wokovu hauchuliwi kana kwamba ni jitihada za Mwanadamu lakini huchukuliwa kama ni thawabu ya Kimungu. Wabaptisti kwa kauli moja husema wokovu haupatikani kwa matendo bali kwa imani.

Kwa hiyo Wabaptisti kwa wingi wao wanakubaliana kwamba ubatizo, ushirika wa Kanisa, meza ya Bwana, na matendo mema, kwa umuhimu wake, lakini sio njia ya kupata wokovu, ni kwa neema kwa njia ya imani yatosha.

“Kusudio la Mungu la neema limejieleza kwenye Biblia nzima.
ni dhahiri, kwamba Maandiko yanafundisha kwamba kusudi la huu ukombozi ni kutoka milele.
Kabla ya uumbaji Mungu mwenye kujua yote alijua kuwa Mwanadamu atatenda dhambi hivyo atahitaji kuokolewa.
Hatahivyo, kitendo cha Mungu kujua kabla haikuwa sababu ya kufanya hivyo. Ilitokana na kutaka kuonyesha uhiari wa Mwanadamu.”
Herschel H. Hobbs,
Mchungaji wa Baptist na Mwana Theolojia
Nukuu kutoka Imani ya Wabaptisi na Ujumbe, chapisho la 2,..uk 55