Uongozi wa Kanisa la Baptist

“Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.”
Wafilipi  2:3

Uongozi wa ushirika chini ya uongozi wa Kristo ni jambo la msingi sana kwa Wabaptisti  kwa kufuata Biblia. Hata hivyo, kuna changamoto mbalimbali siku hizi juu ya hii dhana.

Sababu sababisha juu ya kudhoofika kwa uongozi wa ushirika

Wanaoshuhudia maisha ya Kanisa la Wabaptisti wamebaini changamoto mbalimbali zinazokwamisha huu uongozi wa ushirika. Mfumo wa kuendesha biashara kwa njia ya mkataba umekuwa mfumo wa kuendesha Kanisa.

Mchungaji anakuwa kama Mkurugenzi Mtendaji akiwa na nguvu za kufanya kila kitu yeye mwenyewe haswa kwenye masuala ya fedha, masuala binafsi, uendeshaji wa ratiba mbalimbali za Kanisa na wakati mwingine hata kufanya maamuzi juu ya mtu kujiunga na ushirika. Kwenya Makanisa mengine, kundi fulani, kama wazee wa Kanisa au kamati ya mashemasi, wanatumika kwa mfumo kama huo wa biashaya yenye mkataba.

Mara nyingi inasadikika kwamba kwa kutumia uongozi wa aina hii ni bora zaidi. Maamuzi hufanya na mtu mmoja au na watu wachache  bila umuhimu wa kuwashirikisha watu wengi kwa ajili ya maamuzi, ni kweli, kuna mbinu nzuri za biashara zinaweza kusaidia kwa Kanisa. Lakini kwa uangalifu zisiwe vikwazo kwa ajili ya mwenendo wa uongozi wa Kanisa.

Kuwa na Mkurugenzi Mtendaji na bodi ya Wakurugenzi tunaweza kudhani ni mfumo bora, lakini madhara yake ni kuleta mtafaruko ndani ya Kanisa la Baptist. Matatizo mengi sana yanayotokea ndani ya Kanisa ni kwa sababu ya uongozi, haswa pale Mchungaji anakuwa na maamuzi juu ya kila jambo. Na madhara yake ni kwamba hizi changamoto zinaweza kupelekea kufukuzwa kwa Mchungaji. Makanisa mengi hugawanyika kwa sababu ya hili. Ni kweli, shida sio kwa sababu ya mtu mmoja wala kikundi fulani, lakini sababu ya msingi ni kupuuza uongozi wa ushirika.

Changamoto ya uongozi wa ushirika Mchungaji anaweza asiwe ndio chanzo, wazee wa Kanisa, Mashemasi kuwa na mamlaka lakini kutoka kwa waumini wachache ambao baadae huwa marufu. Kwa mazingira yeyote yale mtu anapopata nguvu ya ushawishi, uongozi wa ushirika hudhoofika.

Baadhi ya sababu zinazodhoofisha mfumo wa Uongozi wa Ushirika Kanisani

Wanaoshuhudia maisha ya Kanisa la Wabaptisti wanaonyesha sababu zingine ambazo zinafanya zinafanya uongozi wa aina hii ya Kibiblia kuwa ni changamoto.

Sababu nyingine ya msingi inaweza ikawa idadi kubwa ya washirika wa Kanisa ambao kiimani hawajakomaa. Uongozi shirikishi na imara wa Kanisa hautegemei tu wale ambao waliokombolewa na Kristo lakini ni pamoja na wale wanaokua kiroho katika Kristo kila iitwapo leo. Watu ambao hawana muda mrefu kwenye hii neema ya wokovu kwa njia ya imani hawatakuwa nay ale mambo yanayohitajika ili waweze kushiriki vema kwenye uongozi shirikishi wa Kanisa, kama vile mtazamo wa Biblia juu ya ukuhani wa muumini na uweza war oho.

Sambamba na hilo, watu ambao hawana muda mrefu kwenye ukuaji wa Kikristo katika njia ipasavyo (1 Wakorintho 3:1-14) wanaweza pia wakakosa sifa ya kuwa na hali ya utumwa unaostahili wakati wakitimiza wajibu wa kumtumikia Yesu kama (Wafilipi 2:5-11).  Utendaji mwema wa uongozi shirikishi wa Kanisa unahitaji watu ambao wana kiu na hamu ya kufuata kusudi la Kristo kwa Kanisa na hutafuta maarifa na hekima kwa waumini makuhani wengine.

Hali ya kutojali na tofauti mbalimbali pia zinachangia kudhoofika kwa utendaji bora wa aina hii ya uongozi kwa ushiriki mchache wakati wa vikao vya kanisa na masuala mengine ya Kanisaa. Kushindwa kuhudhuria kunatengeneza nafasi, kitendo ambacho wale wenye kuonyesha utayari wanapata nafasi ya kuwa na mamlaka ndani ya Kanisa.

Sababu nyingine ya kupelekea kutokuwa na ufanisi kwenye utendaji wa aina hii ya uongozi ni kwa sababu wengine hawaelewi namna gani hufanya kazi uongozi wa aina hii. Ukosefu wa elimu juu ya mafundisho ya Kibaptisti na mwenendo wake umefanya watu wengi kuwa na uelewa kidogo sana wa namna na jinsi ya kuwa na uongozi shirikishi ndani ya Kanisa.

Kwa nini Uongozi Shirikishi ni muhimu

Sababu nyingine ambayo hupelekea aina hii ya uongozi kutokufanya vizuri ndani ya Kanisa ni kwa sababu wengi  hawaoni umuhimu wake wa kipekee. Lakini uongozi shirikishi ni wa maana sanaa.

Uongozi shirikishi ni muhimu kwa sababu unazungumzia jambo muhimu sna juu ya msingi wa Kanisa. Kwa mfano, kushindwa kufuata kile ambavho Biblia inatufundisha kama vile juu ya kuheshimiana huleta swali endapo kweli tunafanya kwa kujitoa juu ya mamlaka ya Neno la Mungu. Kushinda kuwa na aina hii ya uongozi shirikishi ndani ya Kanisa pia huachilia kwamba Kanisa halioni umuhimu wa uweza war oho na ukuhani wa muumini, kwa mtu mmoja au kikundi cha watu fulani kuliongoza Kanisa hushudha hadhi ya haya mafundisho ya msingi.

Uongozi shirikishi ni kuhimu pia kwa sababu husaidia kukuza ukomavu wa Wakristo ndani ya Kanisa. Kushindwa kuwa na aina hii ya uongozi shirikishi pia kudhoofisha ukuaji wa kiroho kwa waumini makuhani kwa kutotoa nafasi kwao ili kuonyesha uweza war oho na uhuhani. Ushirikishwaji wa washirika wote ndani ya Kanisa husababisha Kanisa kukua zaidi na kuibua huduma mbalimbali ndani ya Kanisa ambazo Mungu alizitoa (Waefeso 4:1-15). Hii nafasi sio faida kwa mtu mmoja tu bali kwa Kanisa nzima.

Hivyo, Uongozi shirikishi ni muhimu kwa sababu huchangia ustawi wa Kanisa. Kwa sababu watu huwa na dhana ya kwamba na wao ni sehemu ya Kanisa. Watu wanapojisikia kuwa sehemu ya Kanisa, mara njia wanakuwa na hali ya kujitoa zaidi kwa ajili ya Kanisa. Kuwa na sauti ndani ya Kanisa pia humpa mtu nguvu ya kutoa maoni yake na kusaidia kwenye maamuzi.

Uongozi shirikishi pia ni muhimu kwa  jamii kwa ujumla na sio kwa ajili ya Kanisa tu. Ushiriki wa uhiari wa aina huu ya uongozi hujenga watu zaidi ili kuweza hata kushiriki kwenye masuala ya siasa. Kusema ukweli, siasa za kidemokrasia ni karibia sawa kwa dhana ya Baptist juu ya uongozi shirikishi.

Wana historia wengine husema uongozi shirikishi ulianza wakati ambao maendeleo ya magharibi yalikuwa yakipitia kwenye kipindi cha kuelekea kwenye maisha ya siasa za kidemokrasia. Hivyo walidhani kwamba demokrasia ndani ya Baptist ni kioo tu cha demokrasia ya ulimwenguni kwa hiyo sio kiungo muhimu kwemye maisha ya Kanisa.

Hata hivyo, Uongozi shirikishi wa Baptist hautokani na demokrasia ya kidunia. Ni uongozi ambao msingi wake umetokana na mafundisho ya Biblia.  Ni dhahiri, demokrasia ya kidunia ndio imeiga njia  ya kiroho dhana ya Wabaptisti na wengine ambao wanaamini uhuru na haki ya kila mmoja na wajibu wake kwa kusimamia msingi wa ukweli wa Biblia. Kwa mfano, Mwana historia aliandika miaka ya 1800s kwamba Thomas Jefferson, mwandishi na mwasisi wa Kuutetea Uhuru, alikuwa akishiriki vikao vya maamuzi na mikutano mingine ya kwenye Kanisa la Wabaptisti jirani na nyumba yake, alishuhudia demokrasia kwa vitendo na alitambua umuhimu wa Wabaptisti kwenye kukuza demokrasia ya Wamerakani.

Njia ya kuimarisha Uongozi wa Kanisa Shirikishi

Kwa sababu uongozi shirikishi wa Kanisa ni wa umuhimu kwa sura ya Wabaptisti na ni muhimu kwa ustawi wa Makanisa mengine, kwa mtu binafsi, na kwa jamii kwa ujumla, hatua za madhubuti zinatakiwa kuchukuliwa ili kuimarisha uongozi shirikishi.

Njia mbalimbali zimependekezwa: Jitihada za kusisitiza kila mtu ambaye anataka kujiunga na Kanisa anapaswa kuwa amezaliwa mara ya pili na pia awe Mkristo aliyekomaa Kiroho. Mkazo zaidi uwekwe kwenye uinjilisti na kukua kwa Kristo. Omba kwa ajili ya afya na uhudhuriaji mwema wa washiriki walioko kwenye uongozi. Wafundishe waumini umuhimu wa uongozi shirikishi wa Kanisa na uhusiano wake na mafundisho mengine ya msingi ya Kibaptisti. Wafundishe washiriki jinsi Kanisa la Baptist linavyoendeshwa na muundo wake; dara la wahoji pamoja na mafundisho mengine hili pia linapaswa kuwepo. Liwepo pia kwenye taratibu za kumtafuta Mchungaji na wazee wa Kanisa na  msisitizo juu ya uongozi shirikishi wa Kanisa, ukuhani wa muumini na uweza wa roho.

Nakubali kabisa, Makanisa, haswa yale yenye idadi kubwa ya washirika, wanaweza wakakumbana na changamoto kwenye kuwahusisha washirika wote kwenye uongozi shirikishi. Hata hivyo, kwa njia ya kuwashirikisha kwa njia ya makundi na kamati mbalimbali, kutoa mamlaka kwenye maamuzi mengine ili yafaywe na wao, na kuwa na mkutano wa Kanisa ambao washirika wote watahusika kwenye upigaji wa kura, ni muhimu kuendelea kuwa na msingi wa uongozi shirikishi.

Hitimisho

Uongozi shirikishi wa Kanisa ni suala ambalo liko sambamba na mafundisho mengine ya Wabaptisti ambayo msingi wake ni Biblia. Kila Mbaptisti anayo nafasi ya kushiriki lakini pia kuziendeleza ili ziendelee kutumika na kustawi.

“Japo Wabaptisti kwa kawaida huamini sana dhana ya uongozi shirikishi wa Kanisa, madhara ya yake na ufanisi wake bado yapo – kwa pande zote mbili ndani na nje ya familia ya Kibaptisti.”
Ebbie Smith
Mafundisho Muhimu kwa Baptist