Wabaptist na Elimu

“ Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.”
Zaburi 1:7

Wabaptist huamini upatikanaji wa elimu ya Kikristo kwa watu wote na zipo njia mbalimbali za kuifikishia hii elimu. Husaidia upataikanaji wa elimu ya Kikristo kwa njia ya kutoa msaada wa fedha, muda na vipawa. Dhehebu la Kibaptist ni dhehebu lililojaa mafundisho kweli kweli.

Sababu kwa nini Wabaptist hutoa msaada wa Eimu ya Kikristo

Kujitoa kwao juu ya elimu ya Kikristo kunatokana na msingi wa mafundisho ya Biblia, kama vile imani na mafundisho yao mengine hutokea.

Biblia inaelezea habari za kuimarisha akili na roho pia.  Yesu alifundisha, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.” (Mathayo 22:37).

Akili ya Mungu hupatikana kwenye Biblia. Biblia hueleza, “Jitahidi kuonyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiyekuwa na sababu ya kutahayari, akitumia kwa halali neno la kweli.” (2 Timotheo 2:15). Maandiko hutufanya “kukuhekemisha hata kupata wokovu” (2 Timotheo 2:15). Elimu ilikamilika, hivyo basi, huchochewa na usomaji wa Biblia.

Elimu ya Kikritso sio kusoma Biblia tu, hata hivyo. Kwa maana Mungu ndiye muumbaji wa kila kitu (Mwanzo 1-2; Wakolosai 1:16),  Elimu ya Kikristo ni pamoja na kuielewa dunia jinsi ilivyo na kuielezea kwa mtazamo wa Kitheologia. Hiyo elimu huongeza utashi mkubwa kiakili.

Wabaptist pia hutoa elimu kwa sababu huamini inasaidia kuongeza nguvu na kuimarisha  Makanisa na kutoa mchango mkubwa kwa kuwa na jamii ya haki na mwenendo mzuri. Elimu ya Kikristo sio kwamba inasaidia kuwa na washirika hai ndani ya Kanisa bali hujenga pia jamii yenye mtazamo mwema kwenye jamii

Uhusiano baina ya Elimu ya Theologia na Mfundisho mengine ya Baptist

Mafundisho ya Baptist na mwenendo wao ndicho kinachopelekea kuwa waadilifu kwenye utoaji wa elimu ya Kikristo. Kwa kweli elimu ya Kikrsito huchochewa na mafundisho na mienendo mbalimbali ya Baptist. Kwa mfano, imani ya Wabaptist juu ya kutambua mamlaka ya Kibiblia huwezesha watu kuisoma na kuielewa Biblia zaidi. Elimu ya Kikristo huimarisha haya maarifa.

Imani ya Baptist juu ya uweza wa roho na ukuhani wa waumini kwa wote walioamini ni sehemu ya elimu ya Kikristo. Japo uweza wa roho ni zawadi kutoka kwa Mungu na sio jitihada za kibinadamu, huo uwezo wa kumjua na kumfuata Mungu hutokana na elimu ya Kikristo. Hivyo, elimu ya Kikristo na mafunzo vinaweza kuchochea huduma ya waumini makuhani.

Uongozi shirikishi na utegemezi wa Kanisa la mahali, yote ni mafundisho ya Baptist, huimarishwa na elimu ya Kikristo. Maarifa ya mafundisho ya Kibaptist na mwenendo na namna na kwa nini hivi vililenga kusaidia washirika wa Makanisa kutimiza wajibu wao kwenye majukumu ya uongozi.

Uinjilisti, umisheni, huduma mbalimbali na kuishi jinsi injili inavyosema kwenye maisha yetu ya kila siku haya yote huchochewa na elimu ya Kikristo. Mafundisho na mafunzo hutoa maarifa na akili inayotakiwa kwa watu ili kutimiza hayo majukumu. Uhuru wa kuabudu hulindwa na kumarika kwa watu ambao wamejengwa juu ya msingi wa elimu ya Kikristo ya Biblia na kwenye historia.

Aina ya ELimu ya Kikristo

Wabaptist huwezeshwa upatikani wa mahitaji mbalimbali ikwa ajili ya elimu ya Kikristo, kwa njia rasmi na isiyo rasmi. Huanzisha aina mbalimbali za mashule na watu wa aina mbalimbali ili kupata elimu rasmi. Kwa nyongeza, huwezesha upatikanaji wa majitaji kwa watu mbalimbali ili kupata elimu isiyo rasmi. Watu wengi ambao hawakubahatika kupata elimu rasmi hujifunza vema kwa kutumia nyenzo mbalimbali zilizopo.

Wabaptist huamini kwamba elimu ni kwa ajili ya watu wote. Hutoa upatikanaji wa elimu kwa ajili ya watoto na watu wazima, wanaume kwa wanawake, kwa makabila yote, kwa dini zote na kwa watu wenye uchumi tofauti tofauti. Maelezi juu ya masomo mbalimbali hupatikana kwa njia mbalimbali.

Baadhi ya mafundisho na mafunzo hutolewa kwa ajili ya viongozi wa Kanisa. Dhehebu la Baptist halina kiwango maalum cha elimu kwa ajili ya mtu kusimikwa kuwa Mchungaji na hata kiongozi wa Kanisa. Hata hivyo, kwa kuamini uthamani wa elimu, Wabaptist wameanzisha mashule ili kutoa elimu kwa ajili ya hao watu huku pia ikitambua kwamba wengi wamekuwa viongozi bora kwa sababu ya kupata elimu isiyo rasmi.

Elimu ya Kikrsto kwa watumishi wengine ni muhimu sana kwa Wabaptist. Wabaptist hutazama uwepo wa vyuo vikuu, sio tu kutoa elimu kwa wale watu ambao tayari wapo kwenye huduma ya Kikanisa, lakini pia kwa watu wengine waliopo.

Njia za kupata Elimu ya Kikristo

Wabaptist hutumia njia mbalimbali na mifumo mbalimbali ya jnsi ya kutoa hii elimu. Makanisa, Makanisa ya Majimbo, Kanda na taasis mbalimbali ni mashirika ambayo hujihusisha zaidi.

Makanisa hutoa elimu ya Kikristo kwa njia mbalimbali, kama mahubiri, madarasa ya shule ya Jumapili, kwenye vyuo vya Biblia, idara za wanaume na wanawake, mipango mbalimbali ya mafunzo maalum, maktaba ya Kanisa, makongamano na njia zingine nyingi. Kwa kuongezeea kwenye Biblia na mafundisho mengi na masomo mbalimbali hufundishwa. Makanisa mengi hutoa mafunzo ya kuajiriwa, kama kuajiliwa na kazi za ufundi stadi. Makanisa mengi huendesha shule za chekechea, za msingi na sekondari.

Makanisa ya kwenye majimbo husaidia pia kutoa mafunzo kupitia makongamano, warsha, makambi mbalimbali, na semina. Wengine huwa na mafunzo endelevu kwa ajili ya Wachungaji na viongozi wengine wa Makanisa, mara nyingi kwa kushirikiana na seminari au vyuo.

Kanda na ngazi za Kitaifa za Kibaptist huanzisha taasis kwa ajili ya elimu, kama vile elimu maalum, vyuo vya Biblia, Vyuo vikuu na seminari, kuchagua wasimamizi na kutoa msaada wa fedha. Shule za Baptist hutunuku shahada, astashahada na uzamivu kwenye mafunzo mbalimbali na vyeti vingine.

Shule za Kibaptist hujihusidha pia na uinjilisti, umisheni na huduma. Sio tu kuimarisha wakufunzi kwa ajili ya baadae lakini pia hutoa maeneo ya kufanya huduma kwa vitendo kwa wanafunzi, kitivo na wahudumu ili kutumika hata sasa. Kujishughulisha kwenye masuala hayo huchochea ukuaji wa elimu ya Kikristo.

Wabaptist hutoa majitaji mbalimbali kwa ajili ya elimu, kama vile vitabu, majalada, magazeti, tamthilia, filamu, mengine kwa njia ya mtandao, kwenye cd au kurekodiwa. Makanisa, Majimbo, taasis na mashirika ya Kimataifa husaidia upatikanaji wa haya yote. Kwa kuongezea kwenye elimu madhubuti ya Kikristo, Wabaptist wengi husaidia kutoa elimu kwa namna mbalimbali, kwenye maeneo ya kazi kama serikali, sekta binafsi, shule binafsi na kwenye vyuo mbalimbali.

Changamoto zinazohusiana na Elimu ya Kikristo

Wabaptist hushughulika na changamoto mbalimbali kwenye utoaji wa elimu ya Kikristo. Kwa mfano, kwa mfano, ukuaji mkubwa wa dhehebu na hupelekea kuwa na eneo kubwa kwa ajili ya kuifikisha elimu kwa watu wengi.

Churches confront the challenge of getting people to take part in educational opportunities. Scores of activities clamor for the time of persons, young and old. Church education must be relevant, appealing and accessible in an assortment of ways.

Cvyuo na Seminari hushughulika na masuala ambayo kwa kweli yana changamoto, kama vile uhuru wa elimu, sifa za waalimu, na mambo yaliyomo kwenye mtaala wa kufundishia. Namna bora ya kujumuisha imani ya Kikristo na masomo ni moja la jambo ambalo huleta changamoto kwa Baptist. Ni muhimu kwamba msimamo wa Baptist usiharibiwe but ndio iwe dira ya kutoa elimu bora

Mahusiano ya vyuo vikuu kwa taasis za dhehebu la Baptist, kama vile ngazi ya Kitaifa, huibua baadhi ya maswali juu ya endeshaji na matumizi ya fedha. Kumbukumbu za Kihistoria za shule za Biblia huonyesha kwamba endapo shule zinakosa ushirikiano mwema na ngazi mbalimbali za Kanisa basi hawajishughulishi sana na kulinda mafundisho ya Baptist.

Upungufu wa fedha za uendeshaji wa elimu ya Kikristo limekuwa tatizo la muda mrefu sana. Kama msaada wa dhehebu kwa mashule umepungua, taasis zinaelekea kutafuta njia zingine nyingi mbadala. Hili linapelekea kutokuwa makini kwenye mafundisho na msingi wa Baptist.

Hitimisho

Kwa kiasi kikubwa cha kujitoa Wabaptist wamesaidia sana kutoa elimu mbalimbali kwa Wabaptist na wasio wa Baptist. Kwa kufanya hivyo wamesaidia kuimarisha Makanisa na taasis kwa ujumla. kizazi cha baadae kinapaswa kuendelea huu mfano ambao uliwekwa na Wabaptist wa zamani ambao waliamini sana kwenye elimu ya Kikristo.

“wakati umefika ambapo, haijawahi kutokea, kwa dhehebu letu pendwa kwenda na jukumu lake kwa ulimwengu kama dhehebu lenye mafundisho.
George W. Truett
Mchungaji wa Baptist na Kiongozi wa Dhehebu,
maneno aliyohubiri kwenye ikulu ya Marekani 1920