Wabaptisti huamini katika Ushirika Upya

“Bwana akalizidisha Kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.”
Matendo 2:47

Ni sehemu gani Kanisa lako lilipo? “Jibu la hili swali bila shaka litakuwa ni eneo ambalo majengo yamejengwa. Lakini Kanisa sio jengo. Kanisa ni ushirika wa waumini wanaoishi maeneo tofauti tofauti….kundi maalum la watu.

Ni nani anapaswa kuwa mshirika wa Kanisa?

Wabaptisti wametumia tafsiri mbalimbali kuelezea maana ya Kanisa, kama vile Kanisa la muumini, Kanisa jipya, Kanisa lenye mkusanyiko, Kanisa la hiari, Kanisa la waliookoka na ushirika uliokombolewa.

Haijalishi tafsiri gani inatumika, kimsingi maana yake ni sawa tu: Kanisa ni ushirika wa watu kwa hiari yao wameamua kumfuata Yesu kama Bwana na wanashirikiana kwa hiari chini ya Bwana na kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu.

Hivyo Wabaptisti huamini ni wale tu waliobatizwa ndio washarika wa Kanisa. Wabaptisti pia huamini kwamba watu waliokolewa wanapaswa kuwa washirika wa Kanisa. Wakati suala la kuwa Mkristo ni la binafsi baada ya kuikiri imani, kukua katika Ukristo kunachochewa na ushirika wa pamoja na Wakristo wengine. Maisha ya Kikristo hayakuwa na lengo la kujitenga bali kama ushirika wa pamoja, Kanisa likiwa ndio msingi wa huo ushirika.

Dhana iliyomo kwenye Agano Jipya juu ya Kanisa ni mwili wa waumini waliobatizwa katika Kristo. Hata hivyo, kwenye mistari michache ya Agano Jipya neno “Kanisa” ni wale wote waliokolewa bila kujali umri (Mathayo 16:18; Waefeso 5:23-32; Wakolosai 1:18)

Japo Wabaptisti huamini kwamba ushirika wa muumini ni pamoja na kuokolewa katika Kristo, hutoa wito na kuhamasisha kila mtu kushiriki na kufanya huduma mbalimbali za Kanisa. Kwa mfano, huduma za kuabudu, masomo ya kujifunza Biblia na matukio mbalimbali ya huduma ambazo zii wazi kwa watu wote.

Ni kwanini ni Wale tu Walioamini wanapaswa kuwa Washirika wa Kanisa?

Kwa Wabaptisti Biblia ndiyo kitabu pekee chenye mamlaka juu ya imani na desturi yetu. Wabaptisti huamini katika mafundisho ya Biblia kwamba ni wale tu walioamini ndio wanapaswa kuwa waumini wa Kanisa. Kuzaliwa huku kupya hakuji kwa kutamka tu juu ya Yesu bali kwa kumwamini yeye (Yohana 3:1-21).

Agano Jipya linaeleza kwamba Kanisa ni mkusanyiko wa watu wote waliopata wokovu kwa njia ya kumwamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi. Kitabu cha Matendo ya Mitume kinazungumzia juu ya Kanisa la Yerusalem, “Bwana akalizidisha Kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa” (Matendo 2:47). kwenye nyaraka zote za mtume Paulo kwenye salamu na hata ujumbe wake vinaonyesha kwamba Kanisa ni mkusanyiko wa wale wote waliokombolewa (1 Wakorintho 1:2; 12:12 -31)

Wazo la kusema ambaye ameokoka ndiyo anaepaswa kuwa mshirika wa Kanisa halijazaa matunda sana, hata wakati wa Agano Jipya. Japo kumpata mtu ambaye kweli kweli ameokoka ni ngumu, lakini ni jambo ambalo linapaswa kulifuata na kulichukulia umuhimu wake. Kwa hiyo, Makanisa ya Baptist yanapokea wale washirika ambao wameokolewa.

Ni kwa namna gani Wabaptisti hupokea Washirika wapya kwenye Ushirika?

Uhsirika ndani ya Kanisa la Baptist kila wakati ni wa hiari. Kwa hiyo, watu huomba kuwa washirika. Hawashurutishwi kuwa washirika. Makanisa ya Kibaptisti yanajitahidi sana kwa njia yeyote ile kuweza kuwa na washirika wa Kanisa ambayo kweli wameokolewa.

Kama mtu ambaye hajawahi kuwa mshirika wa Kanisa lolote anaomba kujiunga na Kanisa la Baptist, anauliza endapo anao ushahidi wa kwamba aliwahi kumwamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi. Zaidi ya hapo, Makanisa ya Baptist humshauri huyo mtu kubatizwa kabla ya kufanyika kujiunga ushirika. Kwa hiyo, mtu ambaye anataka kujiunga anaombwa kumwamini Kristo na kubatizwa pia.

Kama mtu ambaye tayari alikuwa amejiunga na Kanisa la Baptist na anatafuta kujiunga tena kwenye Kanisa lingine la Baptist, kwa kawaida huyo mtu huruhusiwa moja kwa moja kwa sababu tayari ni Mbaptisti. Kwa wakati mwingine, makanisa mengine ya Baptist hutoa “barua” yenye maelezo kwamba mhusika wa hiyo “barua” alikuwa mshirika na ameomba kuchukua “barua” anapoenda kwenye Kanisa lingine. Leo hii,, suala la “barua ya kuja”  kwa kawaida huonyesha Kanisa linalopokea mshirika litawasiliana na Kanisa alilotoka juu ya kuhamishwa ushirika. Maana ya “kuja na taarifa” kuna maana ya kwamba Kanisa ambalo mshirika alikuwa akishiriki halipo tena kwa sababu mbalimbali hivyo haina haja ya kuwa na kumbukumbu.

Lakini kivipi endapo mtu ambaye anaomba kujiunga ametoka kwenye Kanisa tofauti na Baptist? Makanisa ya Kibaptisti, kwa kuwa yana uhuru, hutumia njia mbalimbali. Jibu hutegemea msingi wa Kikristo kutoka kwa ambaye anataka kujiunga lakini pia kwa taratibu za Kanisa.

Kwa kawaida, endapo huyo mtu hajabatizwa ubatizo wa maji mengi, Kanisa la Baptist litahitaji huyo mtu kumkiri Kristo na kubatizwa kwa maji mengi kabla ya kujiunga. Kama mhusika alipata ubatizo wa maji mengi, lakini kwa ishara ya kupata wokovu, Makanisa mengi ya Kibaptisti bado yatamhitaji mhusika abatizwe ili aweze kujiunga; hili hufanya ili kuweka bayana kwamba ubatizo, kweli ni muhimu, lakini sio ishara ya kwamba umepata wokovu.

Kama mhusika tayari alibatizwa kwa maji mengi ikiwa ni ishara tu ya kuthibitisha kwamba mhusika amemkiri Yesu kama Bwana na Mwokozi, Makanisa mengine ya Kibaptisti yatakubali ajiunge moja kwa moja. Lakini Bado makanisa mengine yatahitaji mhusika abatizwe akiwa ndani ya Kanisa la Baptist.

Japo baadhi ya Makanisa machache sana ya Baptist yanaweza kukubali kujiunga endapo mtu atamkiri Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi iwe alibatizwa kwa maji mengi kama muumini, lakini mengi hayako hivyo. Makanisa mengi ya Kibaptisti huchukulia suala la ubatizo wa maji mengi kuwa jambo la muhimu sana.

Ni  sababu zipi zingine zilizopo ili kujiunga na Kanisa la Baptist?

Makanisa hutofautiana endapo mtu kwanza abatizwe ndio aweze kujiunga na Kanisa au mara tu baada ya kumkiri Yesu au hata kama muda utapata kufanya hayo. Wengine hubatiza watu mara tu baada ya kukiri, Wengine huhitaji watu, haswa watoto, kupitia kwenye ushauri kwanza kabla ya kubatizwa.

Makanisa mengine huhitaji wote wanaotaka kujiunga wawe na kipindi cha mashauriano ili kujua hali zao za wokovu na kujitoa kwao kuwa mshirika wa Kanisa. Wengine pia hutazamia hawa watu kuwa na darasa lao maalum wa washirika wapya. Mengine mengi hayafanyi moja kati ya hayo.

Wengine  wa Baptist wanapiga kura kama mtu anahitaji kujiunga na Kanisa. Huo ushirika haupigi kura za kujua kama mtu ameokoka ama la. Hilo suala wanasema ni juu yake na Mungu. ila, ushirika wa Kanisa ni kushiriki pamoja na washirika wa Baptist chini ya mwongozo wa Yesu kama Bwana.

Hitimisho

Imani ya kuzaliwa upya ili kuwa mshirika wa Kanisa la Baptist ni msingi wa imani ya Baptist. Hii dhana ni moja kati ya radha za imani na destru ambazo zinafanya “Mbaptisti kuwa Mbaptisti”. Sehemu itakayofuata itazungumzia kwa nini huu utofauti wa Baptist ni muhimu na njia zinazopaswa kufuata.

“Japo Wabaptisti wako sawa na makundi mengine ya Kikristo juu ya imani mbalimbali, msisitizo wetu wa kuzaliwa upya ili uwe mshirika wa Kanisa ni jambo kubwa saana.”
Warren McWilliams
Tafsiri ya Imani ya Wabaptisti