Wabaptist

“Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika pendo.”
Waefeso 4:15-16

“Maana sisi tu wafanyakazi pamoja na Mungu.”
1 Wakorintho 3:9

Dhehebu la Baptist huweli kulielezea na maelezo hafifu. Wabaptist hawako sawa kwenye kuwaelezea vizuri. Wabaptist hawaelezeki, na fundisho moja tu, lakini kwa muunganiko wa mafundisho na mienendo mingi. Kwa ujumla wake, haya huwafanya Wabaptist kuwa ushirika wa kipekee wa Wakristo. Yako mengi ambayo yanaweza kuwaelezea Wabaptist. Lakini kwenye hili somo tutaangalia mafundisho machache tu.

Wabaptisti ni watu gani?

Wabaptist ni watu tofauti tofauti.
Rangu, Wabaptist ni —“weupe, wa kahawia, weuzi na weupe. “awali walikuwa weupe tu”. Kwa sasa Wabaptist ni watu wa rangi zote za wanadamu.

Kiuchumi,  Wabaptist hutofautiana kutoka kwenye mtu wa hali ya chini kanisa mpaka ma bilionea. Wanaishi kwenye nyumba za kawaida na za kisasa zaidi. Huishi kwa kutafutiza na kuishia kwenye kufanya shughuli za kuwaingizia kipato.

 Kisiasa,  Wabaptist kwa kawaida hupatikana maeneo yote. Hutumika kwenye nafasi mbalimbali serikalini lakini pia hukutana na changamoto ya kuteswa .

Kielimu ,  Wabaptist ni kuanzia watu ambao hawajui kusoma mpaka wenye akili sana. Wabaptist ni pamoja na wale ambao hawakupata elimu rasmi na pia wale ambao wamepanda zaidi kielimu na kufika ngazi za juu.

Kidini , Ushirika wa Baptist huabudu kwa njia rasmi na ambayo sio rasmi. Na wako kwenye makundi mbalimbali wenye huria na wenye itikadi za misimamo mbalimbali.

Kiutamaduni , Wabaptist hutofautiana sana. Hutofautiana kwenye ulaji, muonekano na tamaduni. Sio kwa muonekano wa mavazi wala rangi za nywele ndio kunamtambulisha Mbaptist. Wabaptisti huzungumza lugha na ndimi nyingi.

Wabaptist hupatikana wapi?

Wabaptist wanaweza patikana duniani kote.

Wabaptist huishi, huabudu na kuhuduma kwenye nchi za ya mia. Shirika la  Baptist World Alliance(Umoja wa Wabaptist Duniani) ni mfano ambao unaonyesha kumbukumbuka ya uwepo wao, lakini idadi kamili ya Wabaptist ni ngumu kuitambua. Inakadiriwa kwamba karibia Wabaptist million 50 waliobatizwa ni waumini wa Baptist ulimwenguni kote. Na wengine ma miliona zaidi ambao sio waumini lakini hushiriki na kufaidika ndani ya Makanisa yetu.

Umati mkubwa wa Wabaptist uko Kaskazini mwa Amerika.  Huko Marekani, limefanyika kuwa dhehebu kubwa lisilo la Kikatoliki. Lenye mkusanyiko wa mamia ya majimbo, kanda, mashirika, muungani nk, idadi yao ni kuanzia million 35 hadin 40 ya waumini waliobatizwa.

Idadi kubwa ya pili ya Wabaptist hupatikana Afrika, kwa makadirio ni takribani Wabaptist million 7 wanaoishi. Idadi kubwa ya Wabaaptist hupatikana Nigeria, yenye waumini zaidi ya million 2, nay a pili ni Jumhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, yenye waumini wanao kadiriwa kuwa million 2.

Idadi kubwa ya tatu hupatikana huko Asia,  yenye zaidi ya waumini million 4.5. Nchi ya India ina idadi kubwa ya Wabaptist, yenye wastani wa waumini million 2. Makundi mengine makubwa ya Wabaptist hupatikana Korea, Indonesia na Ufilipino.

Idadi kubwa ya nne ya Wabaptist hupatikana Kusini mwa Amerika,  yenye waumini 1.5 million. Idadi kubwa iko Brazil yenye idadi zaidi ya million 1 ya Wabaptist na zaidi ya Makanisa 8,000. Wabaptist hupatikana kwenye idadi ndogo lakini sio sana kwenye visiwa vya Caribbeani, Amerika ya Kati,  Mashariki ya Kati na Ulaya,   pia kuna idadi kubwa ya Wabaptist Uingereza na kwenye nchi ambazo zilijulikana kama Umoja wa Kisoviet.

Dhehebu la Baptist linakuwa ulimwenguni kote. Idadi kubwa ya ongezeka ni Afrika, ya pili ni Asia. Ongezeko ndogo ni kwenye maeneo ya Ulaya na Amerika Kaskazini, maeneo ambayo kulikuwa idadi kubwa ya Wabaptist.

Ni nini Mchango wa  Wabaptist?

Wabaptist sio wakamilifu. Lakini, Wabaptist wamefanya na wanaendelea kuonyesha mchango mkubwa wenye maana. Kwa kawaida kila eneo la maisha limefaidika kwenye hiyo michango. Kwa njia ya Unijilisti na Umisheni,  Mungu amekuwa akitumia Wabaptist kubadilisha maisha ya mamillion ya watu kwa utayari wao wa kuipokea imani na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo Wabaptist wameendela kutoa huduma kwa watu wengi wenye kuumizwa. —kimwili, kiakili, kimawazo, kijamii na kiroho pia. Hospitali za Baptist, vituo vya afya, mashiriki ya kulelea watoto na watu wazima, mashiriki ya kusaidia majanga, vituo vya kutolea ushauri na taasis mbalimbali zenye nia ya kusaidia wale waliovunjika mioyo kimwili na kiroho, kusaidia watu kupata makazi mapya, na kuchangia kuwa na maisha bora kwa watu wote wenye lika, rangi na hali mbalimbali za maisha.  Wabaptist huiishi injili kwa njia mbalimbali ili kusaidia machungu katika jamii,  kama vile umasikini, ukabila, uonevu, mashtaka, njaa, rushwa, unyanyasaji kwa wanawake na watoto, utumiaji wa dawa za kulevya, na unyanyasaji wa kingono.

Wabaptist hutoa nafasi mbalimbali za kusaidia kupata elimu kwa watu wengi.  Kwa kubolesha vitabu vingi, mara kwa mara au kwa njia ya mtandao, Wabaptist husaidia watu kupata maarifa mapya. Kwa kuendesha mashule, vyuo vikuu na seminari. Wabaptist husaidia upatikanaji wa mafunzo ya elimu.

Labda mchango mkubwa sana ambao Wabaptist wameonyesha ni upatikanaji wa uhuru wa kidini na yanayofanana, utengano wa Kanisa na mamlaka za Kiserikali. Wanahistori, wote wasio wa dini na wa dini, wanatambua Wabaptist kuwa ndio viongozi wa mapambano ya uhuru wa kidini, jambo ambalo bado linaendelea.

Kwa nini Wabaptist hufanya kama wanavyofanya ?

Kwa nini Wabaptisyt wamekuwa kutoka kwenye watu kiduchu, walionewa na kuteswa na pande zote mbili mashirika ya kidini na serikali, mpaka kuwa moja kati ya madhehebu makubwa duniani? Kwa nini Wabaptist walitoa hali zao, mali zao na hata maisha yao ili kutoa huduma kwa watu wengine na kupigania upatikanaji wa uhuru wa kidini?

Japo hakuna jibu sahihi ya moja kwa moja kwa haya maswali, kwa nini Wabaptist wamefanya haya chimbuko lake ni kwenye mafundisho ya Kibaptist.  Wabaptist kwa upana wao ni watu tofauti tofauti, lakini kuna baadhi ya mafundisho na mwenendo ambayo huwaweka pamoja.

Sio fundisho moja au mwenendo ambao unaweza kuwaelezea Wabaptist, lakini kwa ujumla wake, hufanya Baptist kuwa dhehebu la kipekee.  Baadhi ya haya mafundisho au imani, kama kumwamini Mungu, hutumika kwa Wakristo wote. Zingine, kama mafundisho juu ya uongozi shirikishi wa Kanisa, pia hupatikana kwenye madhehebu mengine. Hata hivyo, muunganiko wote wa mafundisho, desturi na mwenendo yanayoshikiliwa na Baptist huyafanya Wabaptist kuwa ushirika wa kipekee miongoni mwa Wakristo.

Mafundisho ya Msingi ya Baptist ni pamoja na: Ukuu wa Yesu Kristo, Biblia ndiyo yenye mamlaka juu ya imani na mwenendo, uweza wa roho, wokovu hupatikana kwa hiari baada ya kutubu na kuamini zawadi ya neema ya Mungu kupitia Mwanae, ukuhani wa waumini wote, ubatizo kwa waumini ni kwa njia ya maji mengi tu na kuzaliwa upya (kuokoka), uhiari wa kuwa muumini wa Kanisa.

Msingi wa Mwenendo wa Baptist ni pamoja na: Uongozi shirikishi wa Kanisa, kujitegemea kwa Makanisa ya Baptist, Maagizo Makuu ya Kanisa (ubatizo na meza ya Bwana),  uwepo wa ofisi mbili za uongozi kwa Kanisa (Mchungaji na Shemasi), msaada wa kifedha unaopatikana kwa njia ya kutoa fungu la kumi na matoleo mengine kwa hiari (sio kodi) na taratibu mbalimbali za jinsi ya kuabudu chini ya uongozi wa ukuu wa Kristo.

Mkazo wa mwenendo wa Baptist ni pamoja na:  Uinjilisti, umisheni, huduma mbalimbali kwa jamii, kuiishi kwa namna ya injili isemavyo na elimu ya Kikristo.

Kujitoa kwa Wabaptist kwa ajili ya uhuru wa kidini umechochea kuimarisha kwa haya mafundisho, mwenendo na desturi. Uhiari, sio kwa lazima, kutoweza kuingiliwa kwa haya mafundisho. Hivyo Wabaptist wanaendelea kusisitiza uhuru wa Kanisa kwenye nchi huru.

Hitimisho

Historia ye Baptist ni yenye kufurahisha nay a kusisimua, yenye kujaa uwezo na ushindi, kujitoa na mafanikio, makubaliano na maridhiano. Wabaptist hutofautiana kwa njia nyingi, lakini kwa ujumla hukubaliana kwenye msingi wa mafundisho na desturi.   Ni dhahiri kuwa Wabaptist kuendelea kwao kusimamia haya mafundisho, sio  kwa namna ya uvumilia tu bali watasonga mbele.

“Habari za Baptist ni habari za kuelezeka.”
Kenneth Scott Latourette
Mzamivu Mstaafu wa Umisheni na Ukristo Duniani.
Chuo Kikuu, Yale