Yesu ni Bwana

“…na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.”
Wafilipi  2:11

Neno “bwana” lina maana nyingi sana na tafsiri mbalimbali. Lakini, kama Wakristo, tunakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana kwa sababu tumejitoa kwa  kumtii yeye, upendo wa dhati na uaminifu thabiti kwake kwa sababu ya vile alivyo na pia kile alichokifanya.

Wakristo wote huamini ukweli wa kwamba Yesu ni Bwana, lakini Wabaptisti wana mkazo zaidi kwenye huu ukweli. Wabaptisti huamini kwamba ni Yesu pekee aliye Bwana wa uzima. Hawakubali kwamba mtu fulani au taasis fulani kama bwana kwa Mkristo mmoja mmoja au wa Kanisa. Kwa imani hii, Wabaptisti, kama Wakristo wa kwanza, wamepatwa na mateso na kutengwa kutoka serikali za dunia na hata mamlaka za kidini.

Thamani ya Utiifu wa Wabaptisti kwa kutambua kuwa  Yesu ni Bwana

Kwa nini Wabaptisti huthamini sana kuwa Yesu ni Bwana? Tumelisimamia sana hili kutokana na uthibitisho mbalimbali, ikiwemo ni pamoja na:

(1)  Biblia inatufundisha kuwa Kristo ni Bwana, na Wabaptisti hutazama na kuamini Biblia kama maandiko ya ukweli juu ya imani na mwenendo.

(2)  Mafundisho ya Biblia juu ya uwezo wa roho kwamba kila Mkristo hapaswi kuabudu kitu kingine isipokuwa Mungu- Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

(3)  Msisitizo wa Kibiblia juu ya uwezo wa roho huachilia kwamba Kristo ni Bwana.

(4)  Agano Jipya kama mfano wa Kanisa linatambua kuwa Kristo ni Bwana, na ndiye kichwa cha Kanisa.

Biblia hufundisha kuwa Yesu ni Bwana

Biblia imejitosheleza na maelezo mbalimbali ya kwa nini Yesu ni Bwana wa wote. Yeye ni Mungu, moja kati ya Utatu Mtakatifu. Yesu alisema, “Mimi na Baba tu umoja,” Jesus declared, “ (Yohana 10:30). Kuhusu Yesu, Biblia inasema kwake Yeye, “maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.”  (Wakolosai 2:9 ).

Yesu alikufa msalabani kwa sababu ya dhambi za ulimwengu kwa hiyo anastahili sifa zote na heshima kama Bwana: “Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka” (Ufunuo 5:12).

Yesu alifufukwa kkutoka kwa wafu, kuonyesha mamlaka yake juu ya kifo. Tunapokutana na Yesu Aliyefufuka, tunakiri kama Mwanafunzi wake Tomaso, “Bwana wangu na Mungu wangu!” (Yohana 20:28).

Yesu alipaa kwenda mbinguni, huko amekaa mkono wa kuume wa Mungu Baba akituombea, na atarudi tena na mbingu mpya na nchi mpya, “na uje, Bwana Yesu” (Ufunuo 22:20).

Ni kiasi gani huelezea kuwa Yesu ni Bwana

Biblia huelezea njia mbalimbali ili kuonyesha ni kiasi gani Yesu ni Bwana. Biblia inaeleza kuwa Yesu ni  Bwana wa viumbe vyote: “Ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.”(Wafilipi 2:10-11).

Biblia inatufundisha kwamba Yesu ni Bwana wa kila mmoja. Wengi hukata na wanashindwa kukubaliana na huu kweli, lakini kwa Mkristo kwa kumtambua Yesu ni Bwana ni jambo la kipeke. Kusema ukweli, maisha ya Kristo huanza pale mtu anapomtambua Yesu kuwa ni Bwana: “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka” (Warumi 10: 9).

Biblia pia huelezea kuwa Yesu ni Bwana wa Kanisa. Yesu alisema,  “nitalijenga Kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda” (Mathayo 16:18).  Na Paulo aliandika kuhusu Yesu, “Mungu akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya Kanisa; ambalo ndili mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote…” (Waefeso 1:22-23).

Yesu kama Bwana na Uweza wa Roho

Biblia inatufundisha kwamba suala la kusema Yesu ni Bwana halina pingamizi. Hakuna mwanadamu wala taasis ambayo inaweza ikachukua haya mamlaka ya Yesu kwa Wakristo. Ni kweli,  watu huweza kupata maarifa na uelewa kutoka kwa wengine, lakini ni Yesu pekee mwenye mamlaka yoote kwa Wakristo.

Wito wa kuwa mfuasi wa Yesu ni pamoja na kujua na kufuata mapenzi ya Yesu Kristo kama Bwana. Mafundisho ya Biblia juu ya uweza war oho huonyesha dhahiri kwamba mwanadamu amepewa uweza wa Kimungu wa kujua na kutambua mapenzi ya Mungu. wanadamu sio kama midole. Muumba wao aliwapa uhuru na uhiari wa kuchagua.

Wabaptist hawakubaliani na jitihada binafsi, au kutoka kwa viongozi wa serikali, au kutoka kwenya mashirika ya dini kuonyesha ni yepi mapenzi ya Yesu kwa wafuasi wake. Wabaptist husisitiza uhuru wa kila mmoja kwamba anao uweza na haki ya kupata na kufuata mapenzi yake Yesu kama Bwana. Kama Wanafunzi wa kwanza walivyosema, “Imetupasa kumtii Mungu kuliko Wanadamu!” (Matendo 5:29).

“Kristo pekee ndiye Mfalme, na mtoa haki kwa Kanisa na dhamira.”
John Smyth (b.1570? – d.1612)
Muingereza mmoja, alikuwa Mchungaji  wa Kanisa la Baptist la kwanza huko Uingereza Amasterdam mnamo mwaka 1609. Hii nukuu ni kutokana na maneno ya ukiri ambayo yalileta faida kubwa kwenye kuelezea.

Uhuru wa kuabudu ni kwa sababu ya kusema Yesu ni Bwana

Kitendo cha kusema Yesu ni Bwana kuna maana kwamba watu na Makanisa wapewe uhuru wa kuabudu bila kuingiliwa na serikali au hata vikundi vya dini kwenye masuala ya kiroho na dini. Wabaptist kila wakati wamekuwa wakipinga hizo jitihada, na kusisitiza kuwa Yesu pekee ndiyo Bwana. Kwa sababu hii Wabaptisti wamekuwa wakijitoa na kulipa gharama kubwa sana.

Kwa mfano, mwanzoni mwa miaka ya 1600 1 Mfalme James wa Uingereza alijitangaza kuwa ndiye Mkuu wa Kanisa la Uingereza ikiwa pamoja na Mkuu wa Nchi ya Uingereza. Alitoa amri kwa Makanisa yote kutii kile alichokuwa akiagiza. Thomas Helwys, Mchungaji wa Baptist, aliandika kitabu chenye kichwa kisemacho  AShort Declaration of the Mystery of Iniquity (Kikiwa na maana ya maneno yenye nia ya uovu ndani yake) ndani yake alimwelezea huyo Mfalme kuwa hana mamlaka ya kuwapangia watu au makanisa kitu cha kuamini.

Helwys alimtumia 1 Mfamle James nakala moja akiambatanisha na maelezo binafsi ambapo alisema,  “Mfalme ni mtu wa kawaida tu na sio Mungu hivyo basi hana nguvu juu ya roho zilizo hai kufuata maagizo yake, au kuweka sheria na maagizo mbalimbali ili kutimiza masuala ya kiroho.” Kwa sababu ya hayo maneno ya ukweli Kibiblia, Mfalme alimfunga Mchungaji, na alikufa akiwa gerezani, kwa kukataa kumtambua awaye yote ispokuwa Yesu kama Bwana wa Kanisa.

Huwezi kutenganisha ukweli wa kwamba Yesu ni Bwana na Agano Jipya

Kuna maana gani kwa Mkristo na kwa Makanisa kukubali kuwa chini ya Yesu kama Bwana? Kwa jambo moja tu, nalo ni kwamba waweze kutambua kuwa Yesu kama Bwana. Kanisa ni mali ya Kristo, na sio mali yao. Yeye ni kichwa cha Kanisa, bali wao sio. Hawana mamlaka ya kutawala Kanisa; bali Kristo ndiye.

Kwa ziada, kila mshirika wa Kanisa anapaswa kutambua kuwa anayo nafasi na jukumu la kufanya maamuzi juu ya Kanisa na kuwa chini ya Yesu kama Bwana. Huu ndio mfumo wa Agano Jipya juu ya Kanisa watu hufanya maamuzi juu ya mahali wanapoabudu, mfano kwamba ni nani awe Shemasi na Mchungaji, ni namna gani fungu la kumi na sadaka vitatumika ndani ya Kanisa, na ni jengo gani wanapaswa kulijenga. Na haya maamuzi yote yanapofikiwa tunapaswa kutambua kuwa bado Yesu ni Bwana wa Kanisa.

Pia,  wote ambao ni wanachama wa mwili wa Kristo wanahusika kwenye maamuzi ya Kanisa. Hakuna uongozi wa ubinafsi ndani ya Kanisa la Agano Jipya. Hakuna Mchungaji, baraza la wazee, au mtu binafsi au kundi lolote linalo mamlaka juu ya Kanisa (I Petro 5:3). Yesu ni Bwana pekee kwa kila mtu na kwa Kanisa kwa ujumla. kwa njia ya maombi na kuheshimu maamuzi mbalimbali kama ushirika wa upendo, washirika wakanisa wanapaswa kujua kusudi la Kristo.

Kwa Muhtasari

Kwa kutambua kuwa Yesu ni Bwana ndio msingi wa mafundisho ya Kikristo. Kwa Wabaptist, lina maana ya kipekee na huendana sambamba na mambo mengine yahusuyo imani ya Baptist, mfano kama Mamlaka ya Biblia kama Neno la Mungu, Uweza war oho, Uhuru wa kuabudu, na muundo wa Kanisa ulioundwa kwa mfano wa Agano Jipya.