Wabaptisti: Ubatizo wa Waumini

“Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.”
Warumi 6:4

Waulize ambao sio Wabaptisti (na baadhi ya Wabaptisti!) Ni nini kinafanya wabatisti kuwa watu wa tofauti na watasema, “Ubatizo wa watu wazima kwa kuzamishwa kwenye maji mengi”. Ndiyo, hakuna jambo moja tu linalowafanya Wabaptisti kuwa watu wa tofauti. Kwa nini basi watu wengi hudhani ubatizo wa maji mengi ndio jambo linalowafanya Wabaptisti kuwa watu wa tofauti? Ukweli ulio wazi ni kwamba Wabaptisti ni moja kati ya madhehebu machache ambayo hufanya ubatizo wa maji mengi na hufanya hivyo kama ishara ya kwamba mtu ameokolewa. Na sio kama ni kibali cha kupata wokovu.

Katika karne zilizopita, watawala wote wa nchi na wa Kanisa waliweka vikwazo ili kuwatesa Wabaptisti kwa sababu ya hili jambo. Mbele ya magumu na makatazo yote pamoja na shida ya kubatizwa kwa hiyo njia, kwa nini Wabaptisti kwa kiburi wameshikilia hiyo imani ya kubatiza muumini kwa maji mengi? Jibu linapatikana kwenye msingi wa imani ya Wabaptisti.

Ubatizo ni kwa Walioamini tu

Agano Jipya imeandika kuwa ubatizo ulifuata baada ya kutubu, haukuwa kabla ya kutubu, na hakuwa na umuhimu kama njia ya kupata wokovu (Matendo 2:1-41; 8:36-39; 16:30-33). Kwa sababu Wabaptisti wanafuata Biblia kama ndiyo yenye mamlaka juu ya imani na matendo, tunaamini kwamba ubatizo ni kwa ajili ya wale tu ambao wameweka imani yao kwa Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi.

Zaidi ya yote, Wabaptisti kuonyeza wazi kwamba kwenye Agano Jipya waamuzi wa kumwamini Yesu na kumfuata kama Bwana na Mwokozi ilikuwa kwa hiari. Kwa hiyo, ubatizo ni ishara ya huo waamuzi ambao wakati wote ni kwa hiari.

Kwa sababu ya imani hizi kwa kufuata Biblia, Wabaptisti hawabatizi watoto wadogo. Hili katazo pia limewapelekea kwenye kuteswa. Kwa mfano, Henry Dunster, rais wa kwanza wa chuo cha Harvard, sio aliamuriwa tu kuiacha office yake bali alifukuzwa kutoka Cambridge kwa sababu ya kukataa kuwa watoto wake wadogo wabatizwe kwenye Kanisa lililokuwa chini ya mamlaka ya nchi.

Ubatizo ni kwa kuzamishwa tu

Japo baadhi ya Wabaptisti wa kwanza walifanya ubatizo wa kunyunyizia maji kwa mtu. Wabaptisti walikubaliana kwamba ubatizo wa kuuzamisha mwili wote kwenye maji ndio ubatizo wa Kibiblia. Hivyo basi, licha ya mateso, vizuizi na kejeli, walianza kufanya ubatizo wa kuzamishwa kwenye maji mengi. Leo, hii ndio njia ya ubatizo kwa Wabaptisti wote duniani kote.

Imani ya ubatizo wa kuzamishwa kama njia sahihi ya ubatizo inatokana na sababu mbalimbali zilizobainishwa kwenye Biblia:

  • Neno la Kiingereza “ubatizo” limetokana na lugha ya Kigiriki – lugha ambayo ilitumika awali kuandika Agano Jipya – likimaanisha “kuzamisha”, “kuzama” au” kutumbukizwa.”
  • Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu kwenye mto Yordani kwa kuzamishwa wakati Yesu akianza huduma yake kwa watu (Mathayo 3:13-17; Marko 1:9-11).
  • Wanafunzi wa Yesu wakati wa Agano Jipya walibatizwa ubatizo wa kuzamishwa (Matendo 8:36-39).
  • Kuzamishwa sio tu kusadiki kwamba Kristo alikufa, akazikwa na akafufuka ili kuleta wokovu lakini pia hudhihirisha tumaini letu kwenye ufufuo (Warumi 6:5).
  • Agano Jipya inatufundisha kwamba kuzamishwa ni ishara kwa muumini kwamba amekufa kwenye maisha yake ya awali na yuko hai kwenye maisha mapya ndani ya Kristo (Warumi 6:3-4); Wakolosai 2:11-12).

Ubatizo ni Ishara

Wabaptisti huamini kuwa Biblia inafundisha kamba ni muhimu lakini sio muhimu kwa ajili ya kupata wokovu. Kwa mfano,mwizi pale msalabani (Luka 23:39-43), Sauli akielekea Damascus (Matendo 9:1-8) na watu waliokusanyika nyumbani kwa Kornelio (Matendo 10:24-48) wote walipokea wokovu bila kujali umuhimu wa ubatizo. Kwenye hotuba yake Siku ya Pentekoste, Petro alisema wale wote waliotubu na kumwamini Kristo watabatizwa, sio kwamba ubatizo humpelekea mtu kupata wokovu lakini kama ushuhuda kuwa ameokoka (Matendo 2:1-41).

Hivyo, ubatizo ni ishara na sio sakramenti. Wabaptisti huamini kwamba Biblia inafundisha kuwa ubatizo ni ishara tu yakuonyesha mtu ameokolewa na si kwa maana ya kwamba amepata wokovu. Ubatizo sio maana ya njia ya kupata neema ya wokovu bali ni njia ya kushuhudia kuwa wokovu umepatikana. Hausafishi dhambi bali ni ishara ya kusamehewa dhambi kwa njia ya kumwamini Kristo.

Wakati ubatizo sio jambo la msingi sana kwa ajili ya wokovu, it hatua ya muhimu sana ya kuonyesha unyenyekevu kwa Bwana. Yesu aliwaagiza wanafunzi wake wabaptize (Mathayo 28:19) hivyo ubatizo ni hatua ya kumtii Yesu kama Bwana. Ubatizo ni moja ya njia ambazo mtu hukiri kwa kusema “Yesu ni Bwana”.

Mtu, Mahali, Muda wa Kuwa na Ubatizo

Dhana ya Wabaptisti juu ya ukuhani wa muumini huonyesha kwamba kila muumini kuhani anacho kibali cha kufanya ubatizo, sio tu Mchungaji au mtu ambaye amewekewa mikono. Kwenye Makanisa mengi ya Kibaptisti, hii huduma inakuwa ya Mchungaji au kiongozi wa Kanisa kufanya ubatizo. Baadhi ya Wabaptisti wamesisitiza kwamba ni wale tu ambao “waliitwa kuhubiri” ndio wanapaswa kubatiza.

Kama kuna uwezekano, eneo la watu wengi ni nzuri zaidi kwa Wabaptisti kufanya ubatizo ni aina ya kuungama kwa imani kwenye umati wa watu. Sehemu mbalimbali zilitumika huko nyuma, wengine walikuwa wakibatizwa mtoni, au ziwani. Kwa mfano, Sam Houston alibatizwa kwenye kijito cha maji kilichokuwa jirani na Kanisa la Independence Baptist. Kwa hivi karibuni, Makanisa yameweza kujenga visima vya ubatizo ndani ya majengo ya Kanisa. Maeneo mengine mbalimbali yanaendelea kutumika, kama vile, mabwawa ya kuogelea, ziwani, mtoni, kwenye madimbwi ya maji, kwenye vijito vya maji, hata kwenye ma josho ya wanyama.

Wabaptisti hawana muda maalum wa kufuata kufanya ubatizo isipokuwa ni utayari wa mtu ambaye ametubu. Kwa kuwa ubatizo sio jambo la njia ya wokovu, kuna umuhimu wa kubatizwa mara tu mtu anapomamua kuokoka. Makanisa mengine hayachelewi hupatiza muda huo huo baada ya ukiri mbele za umati wa watu. Wengine wana mtindo wa kumweka kwanza kwenye darasa la wahoji kabla ya kubatizwa.

Wabaptisti huchukulia ubatizo kama jukumu la Kanisa. Ni kweli, Wabaptisti huamini kwamba kila mtu aliyebatizwa tayari anafanyika kuwa muumini wa Kanisa la mahali. Wabaptisti huchukulia ubatizo sio kana kwamba ni jambo binafsi bali ni jambo la jamii ya makuhani waumini. Ambalo ni Kanisa. Kwa maana, ubatizo ni ishara ya agano kati ya mtu aliyebatizwa na Kanisa.

Hitimisho

Wabaptisti, wanaamini sana uhuru wa kuabudu, kwa kuheshimu uhuru wa wengine jinsi wao wanavyofanya ubatizo. Sambamba na hilo, Wabaptisti wanatamani kuendelea ya uhuru wao pia ili kuonyesha kile wanachokiamini

Wabaptisti huko nyuma walipitia mateso makali sana kwa sababu ya kile walichokiamini kuhusu ubatizo wa muumini, hawakulichukulia kuwa jambo jepesi, walifanya kila jitihada ili kuonyesha vizazi vingine kusudi waelewe  na kutambua umuhimu wake

“Kuwa ubatizo ni ibada kwenye Agano Jipya, iliyotolewa na Kristo,
ili ifanyike kwa mtu ambaye ameamini, au wale ambao wamefanyika kuwa wafuasi,
au wamefundishwa, ambao baada ya kuamini, wanapaswa kubatizwa.
“Njia au namna ya kufanya ibada hii ni kwa kuuzamisha mwili wote ndani ya maji…..”
Makala 39 na 40 ya Waliokiri wa kwanza wa Kibatisti kutoka London mwaka 1644