Je Uweza wa Roho ni Utofauti wa Baptist?

“Chagueni hivi leo mtakayemtumikia.”
Yoshua 24:15

Je uweza wa roho ndio jambo la msingi linalofanya Baptist kuwa ya tofauti? Baadhi ya viongozi waelewa wa Baptist, waliopita, wa sasa, hudhani kuwa huu ndio ukweli.

“…Dhana ya uweza wa roho kwenye dini katika Mungu ni jambo lililochangia Wabaptisti kuwa watu wa tofauti kwenye fikra za ulimwenguni….”
E. Y. Mullins (b.1860 – d.1928)
Mkufunzi wa Baptist/Mwana Theolojia

“Kwa sababu ya dhana hii imesababisha chimbuko la Imani ya Wabaptisti….”
Herschel H. Hobbs (b.1907 – d.1995)
Mchungaji wa Baptist/Mwana Theolojia

“Dhana ya uweza wa roho ni zaidi ya fundisho moja, kiukweli, limechimbua mafundisho mengine ya imani.”
H. Leon McBeth (b.1931 – d.2013)
Mchungaji wa Baptist/Mwana Historia

Maana ya Uweza wa Roho

Ni nini maana ya “uweza wa roho”? Maelezo mbalimbali yameelezea hii dhana, mfano kwamba ni uhuru wa roho, uhuru wa fikra na uweza wa roho. Kimsingi maana yake ni uhuru utokao kwa Mungu unaomwezesha mtu kuelewa na kuitikia katika kulitimiza kusudi la Mungu. wabaptisti huamini kwamba Mungu huwapa watu uweza-yaani kuweza-kufanya uchaguzi. Wanadamu sio midoli au vifaa visivyo hai.

Wabaptisti husisitiza kuwa huu uweza sio tu kwa sababu ya utashi wa ubinadamu, bali ni thawabu kutoka kwa Mungu.  kwenye uumbaji, Mungu aliwapa wanadamu uhuru wa kuchagua. Maelezo ya kwenye Kitabu cha Mwanzo huweka bayana kwamba uhuru huu ulibeba na uwajibikaji ndani yake. Tunawajibika kwa yale tunayo chagua. Na Mungu aliweka bayana madhara ya kuwa na maamuzi mabaya na mazuri pia. Kama tunautumia uhuru tulionao katika kumtii Yeye, basi tunao uzima. Lakini kama tunatumia uhuru tulionao kwa kutomtii, basi matokeo yake ni kifo (Mwanzo 1 -2).

Biblia na Uweza wa Roho

Biblia imejaa mifano mingi juu ya uweza wa roho. Biblia pia hutambua ukweli kwamba wanadamu wanao uhuru. Lakini Biblia pia hufundisha kwamba kila uchaguzi mwanadamu anaofanya basi atawajibika mbele za Mungu.

Kwa mfano, thawabu ya Mungu ya Amri Kumi, zililenga uweza wa mwanadamu kuweza kuzielewa na uhuru wa kukubali au kuzikataa. Kwa kuzikubali basi baraka ziliweza kuambatana pamoja, na kwa kuzikataa basi adhabu zilifuata. Lakini kwa njia zote mbili, bado uweza na uhuru wa kuchagua vilikuwepo (Kutoka 20:1-17).

Watu wa Israeli walipewa uhuru wa kuchagua, kuonyesha uweza wa kufanya maamuzi. Yoshua alisema, “Chagueni hivi leo mtakayemtumikia” (Yoshua 24:15). Hii kauli haingekuwa na maana yeyote endapo kusingekuweko uweza na uhuru wa kuchagua.

Mashujaa wa imani kwenye Agano la Kale, kama Elia, Yeremia na Isaya, walikataa kubadili dhamira zao kwa viongozi wa serikali za wakati wao.

Kwa njia mbalimbali, tunaona pia kwenye Agano Jipya juu ya mkazo kwenye uhuru wa roho. Yesu alisema kila mwanadamu anao uweza aliyopewa na Mungu kuamua kumfuata au kutomfuata. Aliweka wazi kwamba watu wanao uhuru wa kuamini au kutokuamini lakini kwa kila njia mtu alipaswa kuwajibika kutokana na hayo maamuzi (Yohana 3:16-21). Wengine waliamini na kumfuata, lakini wengine hawakuamini (Mathayo 19:16-22).

Yesu hajawahi kuingilia uhuru wa mtu au kulazimisha watu wamfuate hivyo hakuingilia uhuru wa roho ya kila mmoja.

Waandishi wa Agano Jipya mara kadha wamesisitiza hii dhana ya uhuru.W kwa mfano, Mtume Paulo aliandika, “Maana kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamira ya mtu mwingine?”(I Wakorintho 10:29).  Na aliwasihi pia Wagalatia, “And he pleaded with the Galatians, “Katika ungwana huo Kristo alituandika huru” (Wagalatia 5:1).

Zaidi ya hayo, viongozi wa Makanisa ya Agano Jipya waliiga mfano huu wa uweza wa roho. Hawakuwai kumlazimisha mtu kumfuata Yesu kama Bwana na Mwokozi. Ni dhahiri, kwamba walikuwa kinyume kabisa na viongozi wa dini na viongozi wa serikali ambao walionekana kusisitiza kuwa wasimwamini Yesu na kuzungumzia habari zake (Matendo ya Mitume 5:17-42).

Vita juu ya Uweza wa Roho

Dhana ya uweza wa roho limekuwa suala la vita kwa sababu mbalimbali. Wengine hudhani hili suala linapunguza enzi kuu ya Mungu. jibu la Mbaptist kwa huu usemi limekuwa kwamba Bwana mwenye enzi alichagua kumwumba Mwanadamu na uhuru wa kuchagua. Biblia nayo imeweka wazi huu mtazamo wa uumbaji wa Mwanadamu, ikisisitiza mambo yote mawili kwamba ni Mungu mwenye enzi na uhuru  wa Mwanadamu.

Wengine wanadhani hili suala la uweza wa roho huchochea mwanadamu kuwa na kiburi na majivuno. Inawezekana, ni kweli, lakini kwa kueleweka zaidi, kunapaswa kuonyesha unyenyekevu, kila uweza wa mwanadamu ni kwa sababu kumetokana na Mungu kama thawabu, ikiwa pamoja na uhuru wa kujichagulia.

Mashtaka mengine juu yah ii dhana ya uweza wa roho kunaweza kuleta kujitenga na ujamaa pamoja na kutotambua umuhimu wa jamii ya waumini.

Muhtasari wa mafundisho ya Biblia juu ya Uweza wa Roho

Kwa ufupi, Biblia imeelezea ukweli halisi juu ya uweza wa roho:

–kila mmoja anao uweza utokao kwa Mungu ili kumtambua Mungu na kufanya mapenzi yake.

–mungu, ambaye ndio mwenye enzi kuu juu ya viumbe vyote, ametoa huu uhuru.

–huu uweza ni thawabu kutoka kwa Mungu na sio kwamba kumeletwa na mwanadamu.

–Kwa maana hiyo Wanadamu wanao uhuru wa kuchagua, sio midole.

– Mungu halazimishi na wala hamlazimishi ili kuendana na kusudi lake, wala imani na hata upendo halazimishi.

–Kwa huu uweza na uhuru vinaambatana na majukumu ya uwajibikaji. Chaguzi zina madhara.

–Katika kutimiza uhuru wa roho, mtu anapaswa kutafuta maarifa zaidi kutoka kwenye jamii ya waumini, yaani wa sasa na hata waliokuweko.

–Kila mmoja anawajibika kutokana na kile alichokichagua. Itikio la imani linapaswa kuwa ndani ya mtu binafsi na sio kupitia kundi la watu ambalo huyo mtu binafsi ni sehemu yao.

–Tawala za Serikali na mashirika ya dini yasishurutishe watu kufuata kanisa fulani, kukiri mapokeo ya aina yeyote au kufuata taratibu zingine za kuabudu. Kufanya hivyo ni kuingilia uhuru wao na utashi walionao na kuondoa kusudio la sura ya Mungu kwa ajili ya viumbe vyake.

Uweza wa Roho na Mafundisho mengine ya  Baptist

Ijapokuwa uweza wa roho  kunaweza kusiwe u tofauti wa Baptist, lakini ni ndio msingi wa mafundisho mengine ya Wabaptisti. Upekee wa Baptisti ni  jumuisho  wa mafundisho mbalimbali ya Baptist pamoja na desturi zao zilivyojikita kwenye Biblia kama chanzo.

Hata hivyo, uweza wa roho hauna uhusiano wa moja kwa moja kwenye mafundisho mengine ya Wabaptisti na kusema ukweli ndio msingi. Kwa mfano, kwa kutazama mamlaka ya Biblia, Wabaptisti wanasisitiza kwamba SHule zote za Biblia, Waalimu na Wachungaji wanaweza kutoa msaada wa kutosha, kila mmoja anao uwezo na wajibu wa kusoma, kutafsiri na kutumia maandiko mwenyewe kwa msaada wa Roho Mtakatifu.

Wabaptisti huamini kwamba Biblia inafundisha kuwa kuokolewa kutoka dhambini na kifo kwa kusamehewa na kupewa uzima wa milele huja kwa njia ya imani tu kwa kuipokea neema yake Mungu kupitia Mwanae. Wabaptisti pia huamini kuwa wanadamu wanao uweza wa kutimiza kusudi la Mungu kwa njia ya imani na kwamba imani hiyo inapaswa kuwa huru. Kwa hiyo, watu wanapaswa kuwa huru kutoka kwenye mamlaka ya Kiserikali na mashirika ya dini kwa kutolazimishwa na kuingilia uhuru wa imani.

Ubatizo wa muumini, ni jambo lingine kubwa ambalo Wabaptisti husisitiza, baada ya uweza wa roho. Ubatizo ni kwa wale tu ambao kwa hiari wamekubali kwa imani hii thawabu ya wokovu kutoka kwa Mungu kwa njia ya imani. Ubatizo usilazimishwe kwa mtu yeyote Yule. Hicho kitendo kinaweza kuondoa uhuru wa mtu wa kufanya maamuzi kutoa kwa Mungu.

Hitimisho

Sababu moja wapo kwa nini dunia na watu wa dini wamekuwa wakiwatesa sana Wabaptisti kwa karne nyingi ni kwa sababu hawaoni maana ya uhuru. Kuogopa kuona watu wana uhuru wao, hulazimisha kila mmoja kujifunga kwenye dini.

Kutokana na jitihada hizo, Wabaptisti wamekuwa wakihamasisha uweza wa roho na kukubaliana na usemi wa Mtume Paulo: “Kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa” (Wagalatia 5:1).

Wabaptisti wataendelea kufanya vizuri zaidi endapo wataendelea kusisitiza kwamba uhuru huu huambatana na wajibikaji. Tuko huru katika Kristo ili tuweze kutumika kwa wengine: “Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo” (Wagalatia 5:13).