Baptists: Ni nini kinachofanya Baptist kuwa Baptist?

“…Mwe tayari ziku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu…”
I Petro 3:15

“Binafsi nina amini  kuwa tu Mkristo inatosha – sihitaji kuwa muumini wa dhehebu lolote lile.”Umewahi kusikia huo usemi? Ni usemi ambao ndani yake unaachilia Utaua (kumcha Mungu), lakini kwa maana nyingine ni kama vile kuna tatizo endapo mtu akiwa ni muumini wa dhehebu fulani la Kikristo.

Ni nini maana ya “Dhehebu?”

Kuna wakati watu hushindwa kutofautisha kati ya “dhehebu” na “taasis ya kidini” “Dhehebu ni muunganiko wa kundi la watu wenye imani na destruri zinazofanana na kuziishi kama zilivyo.Madhehebu, kwa kawaida huanzisha taasis mbalimbali ili kuweza kutimiza mahitaji na mafundisho ya dhehebu husika, lakini hizi taasis sio dhehebu, bali ni sehemu tu ya kutimiza moja ya majukumu yake. Kwa mfano, Jumuiya Kuu ya Baptist Texas, Jumuiya Kuu ya Baptist Kusini mwa Marekani na Umoja wa Wabaptist Duniani sio madhehebu tofauti, bali ni taasis zilizo chini ya dhehebu la Baptist.

Japo baadhi ya watu wangedhani ingekuwa vema zaidi kwa Wakristo wote kuwa na imani za aina moja na destruri za aina moja na kuishi kwazo, lakini haiko hivyo – na haijawahi kutokea. Tangu enzi za mwanzo wa harakati za Ukristo duniani, maoni na mitazamo mbalimbali imejitokeza kama vile mfumo wa Kanisa, njia ya wokovu na maana halisi ya ubatizo.

Madhehebu ni uhalisia uliopo. Haya madhehebu yapo na yanaendelea kustawi. Kiukweli, mengine, kwa mfano dhehebu la Baptist, lina zidi kukua ulimwenguni kote, na madhehebu yana umuhimu wake.Hufanya mabadiliko makubwa sana kwenye maisha ya mtu na hata ulimwenguni mzima. Udhehebu wa mtu ni sehemu yenye uhakika na huleta mabadiliko makubwa sana kwenye maisha ya mhusika. Kwa maana hii ni vizuri kujua mafundisho na desturi mbalimbali za madhehebu.

Ni nini kinachofanya Baptist kuwa ya Tofauti/Kipekee?

Endapo ungeulizwa swali kwamba, “ Ni kitu gani kinacho tofautisha dhehebu la Baptist na madhehebu mengine ya Kikristo?” ungejibuje? Je ni ubatizo wa maji mengi kwa mtu aliyemwamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yake? Je ni ile hali ya kujitoa na ukuhani wa muumini? Je ni hali ya kuvumilia katika imani na uhuru wa kuabudu?

Hayo yote tayari ni mambo ambayo Muumini wa Baptist anayo. Lakini pia Wakristo wa madhehebu mengine pia wanayo hayo mambo, japo kuna utofauti kwenye ufafanuzi wake.

Ukweli ni kwamba hizo sababu hazimfanyi Mbatist kuwa tofauti na Wakristo wa madhehebu mengine. Sasa ni nini kinachomfanya Muumini wa Baptist kuwa Mbaptisti?

Muunganiko wa mafundisho mbalimbali na desturi hutofautisha Baptist na makundi mengine ya Kikristo. Kuna mafundisho mengi na namna mambo yanavyoendeshwa ndani ya Baptist, yaani yenye radha fulani, kila kiungo kina umuhimu wake kwa Baptist, lakini mchanganyiko wake wote kwa pamoja hufanya radha ya kipekee tofauti na makundi mengine ya Kikristo, hakuna kundi lolote la Kikristo ambalo lina muunganiko wa imani na desturi aina moja kama ilivyo kwa Baptist.

Baptist ilikuja na “vionjo” mbalimbali. Kuna  ufafanuzi na maelezo mbalimbali kwenye baadhi ya masuala, kama vile unyakuo (ujio wa mara ya pili kwa Kristo Yesu), aina mbalimbali za jinsi ya kuabudu na muundo wa dhehebu. Lakini Wabaptist wote wana aina moja ya msingi. Japo kuna baadhi ya viungo huongezewa, vinginevyo hilo halifanyi kuwa Baptist. Huwezi ukautumia unga wa mahindi na kuoka  mkate wa ngano na kuacha unga wa ngano kwa ajili ya kuoka mkate, vivyo hivyo, kuacha kiungo muhimu kwenye mapishi ya Baptist, huwezi ukapata Baptist.

Pishi la Baptist

Ni viungo gani muhimu kwenye pishi la Baptist? Kuna masuala mengine ambayo tuko karibia sawa na Wakristo wa madhehebu mengine, kama vile kumwamini Mungu na Yesu Kristo kama Mwokozi. Hata hivyo, mafundisho ya Baptist juu ya masuala muhimu sana hutofautiana na makundi mengine. Kwa mfano, japokuwa makundi yote ya Kikristo huamini kuwa ubatizo ni suala nyeti kwa Mkristo, Baptist huchukulia ubatizo tofauti na wengine wanavyodhania. Wiki zijazo, kwenye huu mfululizo wa masomo tutajadili hizo tofauti na kwa nini kuna umuhimu sana.

Pishi bora la Baptist ni pamoja na imani na mafundisho kadha wa kadha:

–Uungu wa Yesu Kristo

–Biblia kama mwongozo wa imani na mwenendo

–Uwezo wa Roho

–Kuokoka kutoka dhambini na kifo cha milele kwa kupata msamaha na uzima wa milele kwa njia ya imani kupitia Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi ambaye amekuwa zawadi kutoka kwa Mungu kwa neema tu.

–Ukuhani wa kila muumini na kwa wale wote waliomwamini Kristo

–ubatizo wa muumini

–ubatizo na ushirika wa meza ya Bwana kama ishara kuu lakini sio njia ya kuupata wokovu

–kuwa mshirika wa kanisa kwa Yule aliyezaliwa mara ya pili

–uhuru wa kuabudu na yale yanayolingana, kujitenga kwa kanisa na mamlaka ya kiserikali

Kujengwa kwenye msingi wa haya mafundisho na baadhi ya desturi au mienendo hufanya kuwa sehemu ya pishi:

–uongozi wa kanisa chini ya Kristo kama Bwana

–uhuru wa makanisa

–uhiari wa kujitoa kwenye masuala mbalimbali

Uhusiano wa karibu juu ya haya mafundisho na desturi ni kati ya mambo mengi ambayo hutambulisha Wabaptist wengi:

–uinjilisti

–umisheni

–elimu ya Kikristo

–huduma

–kutoa huduma kwa jamii

Ili kuweza kutimiza hayo vizuri, Wabaptist wanayo mifumo  mbalimbali ya umoja zaidi ya ushirika wa mahali, mfano kama umoja wa makanisa, jamii, jumuiya, falagha, ushirika na muunganiko. Wabaptist pia walianzisha taasis mbalimbali kama vile zinazotoa elimu, kuhudumia watoto, kuhudumia wazee na wagonjwa. Kiungo muhimu kwenye hizi huduma zote ni ushiriki wa kujitoa kwa hiari.

Wabaptist wamefanya bidii kwenye kila fundisho, desturi, msisitizo na namna ya kujiendesha kwa kufuata mafundisho ya Biblia. Kiu ya Wabaptist ni kuenenda sambamba kama vile Agano Jipya inavyojieleza kwa muumini mmoja mmoja na kwa Kanisa la mahali japo ambalo kibinadamu linawezekana kwa msaada wa Mungu kwa kufuata maagizo yake na kwa kutiwa nguvu na Roho Mtakatifu.

Ni nini huleta utofauti?

Ni tofauti gani ambayo dhehebu la mtu hufanya? Kuna utofauti mkubwa sana. Wako Wakristo waaminifu kwenye madhehebu mbalimbali ya Kikristo, lakini yako mafundisho ya kipekee ambayo sisi kama Wabaptisti hufanya  sababu tosha za kutufanya kuwa waumini wa hili dhehebu. Kwa mfano, Wabaptisti huamini kwamba wokovu ni kwa neema tu kwa njia ya imani pekee na sio neema/imani pamoja na ubatizo, au kipaimara, au ushirika wa kanisa. Wabaptisti husisitiza kwamba Kanisa la mahali ndilo lenye mamlaka ya kumweka Mchungaji wanaomtaka wao (Kanisa) na sio kuwa na Mchungaji ambaye ameagizwa au ametumwa kwenu na kundi la watu fulani au uongozi fulani.

Kuna umuhimu wa udhehebu wa Baptist? Ndio, kuna umuhimu wake! Dhehebu la Baptist limefanya mabadiliko makubwa na litaendelea kufanya hayo mabadiliko ulimwenguni. Kwa mfano, tuko huru kuabudu kwenye taifa letu kwa idadi kubwa tuwezavyo kwa kujitoa na bila ubaguzi wa aina yeyote kwa mtu ambaye ni wa dhehebu la Baptist. Wabaptisti wamekuwa mashujaa wa kutoa uhuru wa kuabudu kwa watu wote jinsi wanayojisikia bila kupata upinzani kutoka serikalini au kundi lolote la dini. Wameyafanya hayo licha ya kuteswa. Wabaptisti wanaendelea kupambana ili watu wawe na uhuru wa kuabudu duniani kote.

“Kwa vile kanuni za Baptist ni za kipekee kwa Baptist, kila Kanisa la Baptist, na kwa ngazi yeyote ya uongozi, kuanzia mhubiri mpaka mwalimu wa shule ya Jumapili, tunapaswa kuzisimamia, kama jamii iliyolishika Neno, jambo ambalo ni tofauti na makanisa mengine.”
J. B. Gambrell (b. 1841- d.1921)
Mchungaji wa Baptist, Rais wa Chuo Kikuu, Mhariri, Mkufunzi wa Seminari, Kiongozi wa dhehebu/kiongozi Serikalini